NAULI YA UHALIFU SGR INAUMIZA, INAFURAHISHA

KUNA Jambo moja ambalo baadhi ya abiria wanaosafiri kwa Treni ya SGR hawalifahamu au wamekumbana nalo, ambalo lina maumivu kwao,lakini linalinufaisha Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kuchangia pato la Taifa.


‎Jambo hilo ni Nauli ya Uhalifu ambayo ni faini anayotozwa mara mbili ya nauli anakokwenda abiria anayekutwa ndani ya treni bila kuwa na tiketi.


‎Adhabu hiyo humkumba pia mtu yeyote mwenye shida ya kusafiri  baada ya kukosa tiketi, lakini akawaomba wahusika kwa kuwaeleza umuhimu wa kuwahi kufika anakokwenda.


‎Mimi ambaye ni miongoni mwa watumiaji wakubwa wa usafiri huo, nimekuwa mara kwa mara nikishuhudia utozwaji wa faini hiyo ya Uhalifu ambayo ni dhahiri inawaumiza abiria hao.


‎Kinachonifurahisha ni pale ninapoona wahudumu wa SGR wakitumia mashine maalumu kuwakatia tiketi halali, Jambo linaloniaminisha kuwa malipo yaliyofanyika hayaendi mifukoni mwao, bali yanaingia Serikalini.


‎Siku moja nikisafiri kutoka Dodoma kwenda Dar, nilishuhudia abiria mmoja mwanaume aliyepandia Gulwe kwenda Morogoro akiwa na mtoto wa kike wa umri wa miaka 6, ambaye hakuwa na tiketi, akilipishwa faini hiyo.


‎ Abiria aliambiwa kuwa sheria SGR hairuhusu mtoto wa umri huo kusafiri bure, bali anayeruhusiwa ni mtoto chini ya miaka minne na kwamba zaidi ya umri huo yapaswa alipe nusu nauli na kupatiwa kiti.


‎Ndipo kwa shingo upande alilipa faini hiyo na kupatiwa tiketi. Likaja zogo lingine la kumtenganisha yeye na mtoto ambaye alitafutiwa kiti mbali na yeye, Jambo ambalo hakukubaliana nao kwani yeye alitaka ampakate Ili awe pkaribu naye kwa uangalizi wake, lakini alikataliwa kwa kuelezwa kuwa sheria haziruhusu.

‎Adhabu nyingine anayokumbana nayo abiria huyo mhalifu' ni kukosa kiti hadi kitakapoachwa wazi na abiria mwingine atayeshuka kituo cha jirani.


‎Licha ya kulipishwa faini hiyo, wahudumu wamekuwa wakionekana kuwa wakali na hawapendezwi na tabia hiyo ya abiria kukutwa kwenye treni bila tiketi, kwani sheria za SGR haziruhusu, lakini pia haitakiwi abiria kusafiri bila kuwa na kiti.


‎Akielezea hatua zaidi zinazochuliwa kwa abiria anayepanda treni ya SGR na kukaidi kulipa faini hiyo ya uhalifu, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Fred Mwanjala amesema kuwa;


‎Kwa mujibu Sheria ya Reli namba 10 ya Mwaka 2017 iliyounda  Shirika la Reli Tanzania (TRC), ni kwamba ni marufuku abiria yeyote kupanda treni bila tiketi au kukutwa na tiketi feki na akibainika atalipishwa faini na endapo atakaidi atakamatwa na kukabidhiwa kwa Askari Polisi wa Kitengo cha Reli ambao wamo ndani ya Treni.


‎Amesema kwa kuwa kosa hilo ni la kijinai, mtuhumiwa atapelekwa Mahakamani  kwa hatua zaidi za kisheria.


‎IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MAPACHA WATATU FAMILIA YA MWAIKENDA WAPATA KIPAIMARA

MVUA KUBWA KUNYESHA MIKOA 20

๐Œ๐‰๐”๐„ ๐Š๐€๐‚๐‡๐„๐‘๐Ž ๐Œ๐™๐„๐๐€

AINA 4 ZA WANAWAKE WASIOWEZA KUDUMISHA NDOA.

NAMNA YA KUTENGENEZA MAISHA YAKO KIMYA KIMYA

Wasifu wa Kizza Besigye

NAPE AWAPA UKWELI VIJANA

HAKUNA DHEHEBU LA DINI AMBALO LIKO JUU YA LINGINE, MADHEHEBU YOTE YAKO SAWA KISHERIA - RAIS SAMIA