WADAIWA SUGU WA VIWANJA DODOMA KUNYANG'ANYWA

Halmashauri ya Jiji la Dodoma imetoa notisi ya siku 21 kwa wadaiwa wa viwanja katika maeneo ya Mtumba Zone II, Mtumba Zone III na Kikombo, vyenye Jumla ya thamani ya Shilingi billion 55.4 baada ya kutangaza orodha ya awali ya wadaiwa kufuatia zoezi la uhakiki wa malipo ya viwanja hivyo huku ikisisitiza kuwa viwanja ambavyo malipo yake hayatakamilika baada ya muda huo vitarejeshwa sokoni.

Akizungumza  Desemba 29, 2025 jijini Dodoma, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya jiji la Dodoma, Dennis Gondwe, amesema zoezi hilo limebaini kuwepo kwa watu binafsi, taasisi na kampuni ambazo hazijakamilisha, malipo ya viwanja walivyopatiwa na halmashauri.

Amesema katika maeneo ya Mtumba Zone II kuna jumla ya viwanja 1,915 vyenye thamani ya shilingi bilioni 28.8, Mtumba Zone III kuna viwanja 2,594 vyenye thamani ya shilingi bilioni 20.6, huku eneo la Kikombo likiwa na viwanja 2,051 vyenye thamani ya shilingi bilioni 5.9, ambapo jumla ya thamani ya viwanja vyote ni shilingi bilioni 55.4.

Gondwe amesema kuwa kutokamilika kwa malipo ya viwanja hivyo kumeathiri utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ufunguzi wa barabara, usambazaji wa maji na umeme pamoja na utoaji wa huduma za kijamii kupitia bajeti ya Halmashauri.

Aidha Halmashauri ya Jiji la Dodoma imewataka wadaiwa wote kujitokeza ndani ya siku 21 kukamilisha malipo yao, huku waliolipa lakini majina yao kuonekana kwenye orodha wakitakiwa kufika Halmashauri na nyaraka halisi za uthibitisho.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MAPACHA WATATU FAMILIA YA MWAIKENDA WAPATA KIPAIMARA

๐Œ๐‰๐”๐„ ๐Š๐€๐‚๐‡๐„๐‘๐Ž ๐Œ๐™๐„๐๐€

MVUA KUBWA KUNYESHA MIKOA 20

AINA 4 ZA WANAWAKE WASIOWEZA KUDUMISHA NDOA.

NAMNA YA KUTENGENEZA MAISHA YAKO KIMYA KIMYA

Wasifu wa Kizza Besigye

NAPE AWAPA UKWELI VIJANA

HAKUNA DHEHEBU LA DINI AMBALO LIKO JUU YA LINGINE, MADHEHEBU YOTE YAKO SAWA KISHERIA - RAIS SAMIA