🌿
Imeandaliwa na TIBA
🥬 Majani unayoona mbele yako ni majani ya viazi vitam.
Nafikiri wengi wetu tunawafahamu viazi vitam. Kwa wale ambao hamjui, kwa Kiingereza vinaitwa Sweet Potatoes.
Sasa leo natamani tujifunze faida tano muhimu za haya majani.
Kwanza, ni vizuri kufahamu kwamba watu wengi tumekuwa tukitumia matembele, ambayo yanafanana sana na haya majani, lakini si yale yale.
Zote ni nzuri, ila haya majani ya viazi vitam yana faida za kipekee sana. 🌱
🍠 Viazi vitam vyenyewe ni chakula kizuri sana, hasa kwa watu wenye tatizo la kisukari, kwa sababu husaidia kurekebisha kiwango cha sukari mwilini.
Lakini leo hatuzungumzii viazi, bali majani yake — ambayo wengi hawajui kwamba nayo ni dawa tosha kabisa.
Basi bila kupoteza muda, hebu tuangalie faida tano kubwa za majani ya viazi vitam 👇🏽👇🏽
1️⃣ Huimarisha Kinga ya Mwili 💪🏽
Majani haya ni mazuri sana kwa kuongeza kinga ya mwili.
Kama CD4 zako au mfumo wako wa kinga hauko vizuri, majani haya yatakusaidia kupandisha kinga ya mwili wako na kukuweka imara dhidi ya magonjwa.
2️⃣ Yana Wingi wa Vitamini A 👀 — Afya ya Macho
Majani haya yana vitamini A kwa wingi sana.
Kama unapata matatizo ya macho au kuona hafifu, tumia majani haya mara kwa mara.
Yataboresha macho yako na kusaidia kuyaweka kwenye hali nzuri. 🌿
3️⃣ Husaidia Kusafisha na Kuongeza Damu 🩸 (Detox)
Kama una upungufu wa damu (anemia) au unataka kusafisha damu yako, majani haya ni tiba bora kabisa.
Yana madini ya chuma (iron) ambayo ni muhimu sana katika kutengeneza damu.
Kwa hiyo, kama damu yako ni kidogo au haiko safi, majani haya yatakusaidia kurekebisha tatizo hilo vizuri sana.
4️⃣ Huboresha Mfumo wa Umeng’enyaji 🍽️
Kama unapata matatizo kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, kama vile tumbo kujaa gesi, choo kigumu, au kuhisi uvimbe baada ya kula — basi majani haya yatakusaidia sana.
Husaidia kusafisha tumbo na kufanya mfumo wako wa umeng’enyaji ufanye kazi vizuri. 🌿
5️⃣ Husaidia Kuondoa Sumu na Kuvimba Mwilini ☠️➡️💚
Majani haya yana uwezo mkubwa wa kuondoa sumu mwilini.
Kama umekula chakula kilichokuwa na sumu au umetumia dawa nyingi za kizungu kwa muda mrefu hadi zimeleta madhara, majani haya yatasaidia kusafisha mwili wako na kupunguza uvimbe.
🌿 JINSI YA KUTUMIA
Unaweza kuyatumia kwa njia mbili:
1. 🥤 Kuyablend kama juisi, kisha unakunywa.
2. 🥬 Kuyachemsha kidogo — usiyaache yachemke sana; yakibaki na ile rangi ya kijani kibichi, ndiyo vizuri zaidi.
Unaweza kuweka chumvi kidogo ili kupata ladha.
🍽️ Kula mchemsho huu mara kwa mara, utaona mabadiliko makubwa kwenye afya yako.
Kwa hiyo rafiki yangu 💚
Kama ulikuwa hujui faida za majani ya viazi vitam, sasa umejua.
Anza kuyatumia wewe na familia yako, hakika utashuhudia afya njema zaidi. 🌿✨
https://chat.whatsapp.com/H1uwO14QMwr59wN7H9wFL4

Comments