"Tunatambua kuwa tunacheza dhidi ya klabu kubwa zaidi Afrika, klabu ya karne na hilo linahitaji heshima. Lakini kama tunataka kuwa sehemu ya historia ya soka la Afrika, si suala la kuwa na hofu ni suala la kucheza mpira. Mwisho wa siku tunakuja kucheza na kujaribu kuwashinda wapinzani wetu, huo ndio mpango wetu wa kesho.
Ili ufikie kiwango cha juu lazima ucheze dhidi ya timu bora. Tunaamini kikosi chetu kina ubora, wachezaji wana kiwango na wana hamu ya kutoa kila kitu kwa ajili ya timu. Tunawaamini wachezaji wetu na tunaamini kuwa kesho tutapata matokeo tunayoyataka" Kocha mkuu Pedro Goncalves
#timuyawananchi
#daimambelenyumamwiko

Comments