MFALME WA MOROCCO AKUBALI YAISHE


Mfalme Mohammed IV wa Morocco amesema ana imani kuwa mahusiano ya kindugu na mshikamano wa Kiafrika yataendelea kudumu na hatimaye kushinda, licha ya matukio aliyoyataja kuwa ya kusikitisha na ya kulaaniwa yaliyojitokeza katika dakika za mwisho za fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Morocco na Senegal.

Fainali hiyo ilichezwa Jumapili na iligubikwa na sintofahamu na mvutano mkubwa baada ya waamuzi kutoa penalti kwa Morocco, uamuzi uliopingwa vikali na wachezaji wa Senegal. Kufuatia uamuzi huo, wachezaji wa Senegal waliondoka uwanjani kwa muda kama ishara ya kupinga, kabla ya kurejea na hatimaye kuwashinda wenyeji Morocco kwa bao 1-0 baada ya muda wa nyongeza.

Tukio hilo lilichochea hasira miongoni mwa mashabiki, ambapo makundi ya wafuasi wa Senegal yalijikuta yakikabiliana na vikosi vya usalama vya Morocco walipokuwa wakijaribu kuingia uwanjani kueleza hisia zao kufuatia uamuzi huo tata wa penalti. Hali hiyo ilisababisha sintofahamu na taharuki ndani na nje ya uwanja.

Saa chache baada ya filimbi ya mwisho, mitandao ya kijamii katika nchi zote mbili ililipuka kwa mijadala mikali, majibizano ya maneno, lawama na hisia kali za ushabiki, hali iliyoashiria ukubwa wa mvutano uliotokana na mchezo huo wa fainali.

Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na Ikulu, Mfalme Mohammed IV alieleza kuwa fainali hiyo ilichafuliwa na matukio ya kusikitisha pamoja na tabia alizozitaja kuwa za kulaaniwa, akisisitiza kuwa hali hiyo haipaswi kufuta historia ndefu ya mshikamano na udugu uliopo kati ya mataifa ya Afrika. Ameeleza kuwa mara tu hasira na mihemko itakapopungua, busara na maadili ya Kiafrika yatarejea, na udugu wa bara hili utaendelea kuwa juu ya tofauti za muda mfupi.


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AINA 4 ZA WANAWAKE WASIOWEZA KUDUMISHA NDOA.

MVUA KUBWA KUNYESHA MIKOA 20

MIKOA 10 YENYE KIPATO KIKUBWA ZAIDI KWA MTU MMOJA MMOJA

BODABODA ALIPWA PIKIPIKI BAADA KUSAFIRI KWA BODA KWA SAA 10 MBEYA HADI DAR

IJUE HISTORIA YA MCHEZAJI MZUNGU WA TANZANIA