Naikumbuka sana safari ya Ureno kwenda kuwa Bingwa wa kombe la Euro 2016, naiona safari ya Taifa Stars ikiwa hivyo.!
Mwaka 2016 Ureno licha ya kuwa na watu kama Cristiano na Luis Nani lakini bado haikuwa timu tishio kwenye michuano ile, historia iliwahukumu Kwamba hawajawahi kubeba licha ya kuwa na wachezaji bora kwa vipindi tofauti.
Mechi za makundi zote akasare na kuwa wa tatu kwenye kundi lake akiwa na point 3, akabebwa na uwepo wa Best Loser akaingia 16 bora. Bado akaonekana mwepesi.
Akakutana na Croatia 16 bora akapata ushindi mwembamba akaenda robo, watu wakasema safari imeisha. Wakakutana na Poland ambayo haikuwa tishio saana ila wakasare then akapita kwa penalty, wakasema bahati. Mwanaume kuingia nusu fainali akakutana na Wales ya moto sanaa ya kina Gareth Bale wakashinda 2-0 wakaenda Fainali.
Hapo walikutana na Ufaransa ambao walikuja kuwa mabingwa wa World Cup 2018. Hawa ndio kila mtu alikuwa akiwaona kuwa mabingwa wa Euro 2016, Ufaransa ilisheheni kila idara, kwa Africa ni kama Morocco ya leo. Ni sisi mashabiki wa Ureno ndio tuliamini Ufaransa anakufa ile mechi. Dakika ya 25 tu Cristiano anaumia anaingia mshkaji wake Ricardo Quaresma. Dakika 90 Ngoma 0-0 inaenda extra time mwanaume wa kuitwa Eder anaweka dakika ya 109 Ngoma inaisha dakika 120 Ureno anaongoza moja na anakuwa bingwa kwa mara ya kwanza kwenye historia yao.
Hii inanipa moyo mimi shabiki wa Stars, Mtanzania kuamini tunaenda Robo fainali.! Tunamtoa Morocco.
Historia zipo ili zivunjwe na mpya ziwekwe. Ila mimi naamini tunaweka Historia mpya na tunaenda kuishangaza Afrika na kuchana mikeka.



Comments