Rais wa Urusi Vladimir Vladimirovich Putin anatajwa kuishi nchini Tanzania kwa miaka minne mfululizo tangu mwaka 1973-1978 katika oparesheni za kupigania uhuru wa baadhi nchi za Afrika
Kwa mujibu wa historia, Bagamoyo ilikuwa mongoni mwa vituo vya kuwahifadhi wapigania Uhuru wa Afrika ambapo Putin anatajwa kuwepo katika kituo hicho mwaka 1973 , hapa utaona picha zikimuonesha Putin akiwa na baadhi ya wapigania Uhuru wa Afrika wakiwa katika viunga vya Kaole, Bagamoyo mkoani Pwani.
Mbali na Putin pichani unamuona Rais wa sasa wa Zimbambwe, Emmerson Munangagwa, pamoja na Rais wa Kwanza wa Msumbiji, Hayati Samora Machel
Wapigania uhuru wengi wa Msumbiji na Afrika Kusini walifichwa katika maeneo ya Mazimbu Morogoro na Kaole Bagamoyo yote ni maeneo yaliyyopo Tanzania (Tanganyika zamani).
Urusi na Tanzania zimetajwa kuwa na uhusiano wa karibu tangu enzi za uongozi wa Rais wa Kwanza wa Tanzania, Julius Nyerere, kiasi kwamba madaktari wengi wa Tanzania katika karne ya 20 walichukuliwa na kwenda kusoma Moscow, Urusi.

Comments