Askofu Mkuu wa Makanisa ya Karmeli Assembilies of God (KAG) Tanzania, Dkt. Evance Chande amewasihi viongozi wa dini na watanzania kwa ujumla kuacha mijadala ya kidini isiyofaa inayoendelea kwenye mitandao ili Taifa lisije likafikishwa pabaya na hatimaye kuangamizwa.
Askofu Chande ametoa wito huo wa Tahadhari katika ibada maalumu ya kuukaribisha Mwaka Mpya 2026 katika Kanisa la KAG Ipagala jijini Dodoma Januari Mosi, 2026.
Katika Ibada hiyo aliwaombea pia vijana, Wakulima, Wafanyabiashara, Wafanyakazi,Wanafunzi, Watoto na Watanzania wote kwa ujumla.

Comments