Rais wa Marekani Donald Trump amesema anataka kila mtu awe ndani ya Bodi yake ya Amani huku akihakikisha kuwa Rais wa Urusi Vladmir Putin amekubali kujiunga na bodi hiyo.
Akinukuliwa na CNN jana Jumatano, Rais Trump amesema: “Tunataka kila Mtu awe ndani ya Bodi ya Amani japo nafahamu nimealika Watu watata sana ila tunawahitaji sana ili kukamilisha hii kazi na ndio aina ya Watu wanahitajika humu.
Humu sio pa kujaza Watoto tupu tunahitaji Wanaume wenye ushawishi kama Putin.”

Comments