Muonekano wa visima vinne vya kuhifadhi Mafuta karibu gati ya kuegeshea meli kwa ajili ya kupokelea mafuta eneo la Chongoleani Tanga. Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kwa upande wa Tanzania umefikia asilimia 79 na unagharimu dola za Marekani bilioni 5.
Mradi huu unakwenda kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kuzalisha ajira za moja kwa moja na zisiizo za moja kwa moja na kuwanufaisha Watanzania kupitia fursa mbalimbali zinazotokana na mradi huo.

Comments