JE, USHAWAHI KUONA "JICHO LA KIJANI" LA BUSOKELO?

Mbeya ni mkoa uliobarikiwa, lakini ukienda ndani kabisa kule Busokelo, kuna siri moja nzuri ambayo asili imeificha katikati ya kuta za kijani. Hilo si lingine bali ni Ziwa Itamba

maarufu kama "Ziwa la Ajabu" 
Maajabu ya Asili 
​Kijiolojia, Ziwa Itamba ni Crater Lake. Maelfu ya miaka iliyopita, ardhi ilipasuka na kutoa moto wa volkano, kisha kilele chake kikashuka na kutengeneza duara hili kamilifu. Leo, badala ya moto, kuna maji ya bluu tulivu yaliyozungukwa na msitu mzito. Ni kama mchoro wa gharama uliowekwa katikati ya Milima 
Siri na Utulivu wa Kitamaduni
​Ukiuliza wazee wa kienyeji, watakuambia Ziwa Itamba lina "pumzi" yake. Kwa jamii ya Wanyakyusa wa Busokelo, hapa ni eneo la utakatifu. Ni mahali ambapo ukimya unazungumza. Kuna simulizi za kale za mizimu ya mababu wanaolinda amani ya ziwa hili. Sio mahali pa kelele, ni mahali pa kutafakari na kuungana na uumbaji.
Pana Mandhari ya kipekee Kwa wapenzi wa pichaa Ziwa Itamba linakupa muonekano wa mandahari ya tofauti 
Pana Hewaa Safi Harufu ya miti na upepo mwanana kutoka milimani itakufanya usahau msongamano wa mjini  Safari ya kufika hapo ni burudani tosha kwa wapenda mazoezi na utalii wa ndani.
​Busokelo ni sehemu ya paradiso iliyopo hapa hapa Mbeya

Je wewe ni mwenyeji wa Mbeya na hujawahi kufika hapa? Je  ungetamani kwenda na nani?

​📍 Location: Busokelo, Mbeya - Tanzania.
#UtaliiWaNdani #MbeyaYetu #Busokelo #ZiwaItamba #TanzaniaUnforgettable #NatureLovers #MbeyaCity

Tonny Alvin 
04/04/2026


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

OWM–TAMISEMI YASHINDA TUZO YA MABADILIKO YA KIDIJITALI KATIKA TEHAMA AWARDS 2026

NI MAKOSA WANAFUNZI KUFIKA SHULE SAA 1:15 ASUBUHI

MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU

VIONGOZI NA WATENDAJI WA MATAWI UVCCM PANGANI WANOLEWA

NMB YAWAUNGANISHA WANANCHI NA HUDUMA, FURSA ZANZIBAR