MWIGOMBE TECHNICAL SECONDARY SCHOOL: Wanakijiji wanaendelea na ujenzi


Jimbo la Musoma Vijijini:
Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374

*Idadi ya Sekondari: 30
*Idadi ya Sekondari mpya  zinazojengwa na wanavijiji: 12

Kata ya Kiriba:
Kata hii yenye vijiji 3, imeamua kila kijiji kiwe na sekondari yake:

(i) Kijiji cha Bwai Kwitururu:
Kiriba Sekondari iko kwenye kijiji hiki. Sekondari hii inasubiri maji ya bomba kuanzisha "high school" ya masomo ya sayansi.

(ii) Kijiji cha Bwai Kumsoma:
Bwai Sekondari imejengwa kwenye kijiji hiki. Ujenzi wa kuongeza miundombinu ya elimu unaendelea. 

(iii) Kijiji cha Kiriba:
Mwigombe Technical Secondary School inajengwa ndani ya kijiji hiki. Ujenzi umeanza kwa kutumia michango ya fedha na nguvukazi za wanakijiji.

Wazaliwa wa kijiji hiki wanatoa michango mikubwa ya fedha kwenye ujenzi huu.

Wadau wa Maendeleo, hususani, Benki za NBM na CRDB zimeanza kuchangia ujenzi (rejea taarifa ya awali)

Mbunge wa Jimbo ameanza kutoa mchango wa Saruji Mifuko 200.

Maendeleo ya ujenzi wa Mwigombe Technical Secondary School:

(i) Boma la vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja limekamilika: angalia picha

(ii) Boma jingine la vyumba viwili vya madarasa na ofisi limeanza kujengwa - angalia picha

OMBI:
Wanakijiji wa Kiriba wanaendelea kukaribisha michango ya fedha na ya vifaa vya ujenzi kutoka vyanzo mbalimbali - karibu tuchangie ujenzi wa sekondari ya ufundi ya kijijini Kiriba.

Picha zilizoambatanishwa hapa:
(i) Boma la kwanza lililokamilishwa
(ii) Boma la pili lililoanza kujengwa wiki iliyopita

Ofisi ya Mbunge 
Jimbo la Musoma Vijijini 
www.musomavijijini.or.tz 

P. O. Box 6
Musoma

Date: Tue, 7 April 2026




 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Wasifu wa Kizza Besigye

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

KATI YA WATOTO 7 WA HAYATI MAGUFULI ANAYEJULIKANA ZAIDI NI JESCA

KIKOSI KILICHOITWA TAIFA STARS HIKI HAPA

KWA KHERI MAKARANGA UMEUTIMIZA MWENDO...

UBORA UNAONEKANA: BENKI YA NMB YANG'ARA TUZO ZA EUROMONEY 2026

WANAJESHI WAGOMA KWENDA IRAN KUPIGA

MCHIMBAJI MDOGO WA DHAHABU AFANYA MAKUBWA KWENYE HUDUMA ZA AFYA