SERIKALI imeamua kuanzisha Mfuko Maalumu utakaosaidia kupunguza makali ya bei ya mafuta ambayo imepanda kufuatia vita vinavyoendelea kati Israel, Marekani na Irani.
Mpango huo umeelezwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika Makao Makao ya CCM.jijini Dodoma Aprili 7, 2026.
Amesema kuwa CCM na Serikali itahakikisha mafuta yanapatikana wakati wote na kwa bei nafuu.
Aidha, Kihongosi amesema kuwa Serikali pia ina mpango wa kutoa ruzuku katika mafuta kama ilivyofanya wakati wa vita vya Urusi na Ukraine ambapo Serikali ilitoa bil. 100.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0715264203

Comments