Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hamza Hassan Juma amesema Zanzibar haina ubaguzi kwa wananchi wa Tanzania Bara, akisisitiza kuwa pande zote mbili zimechangamana kijamii na kiuchumi kupitia Muungano.
Akizungumza leo katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati wa mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Hamza amesema kuna upotoshaji unaodai kuwa watu kutoka Tanzania Bara hawapati huduma sawa visiwani humo.
Amesema madai hayo si ya kweli, akieleza kuwa wananchi wa pande zote wamekuwa wakiishi na kufanya shughuli zao katika maeneo yote ya Muungano bila vikwazo.
“Kuna wanaopotosha kwamba watu kutoka Bara hawatibiwi, sio kweli. Zanzibar hakuna ubaguzi,” amesema Hamza.
Ameongeza kuwa Watanzania wa Zanzibar wamejenga familia katika maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara, na pia wananchi wa Bara wanaishi na kufanya kazi Zanzibar, jambo linaloimarisha mshikamano wa Muungano.

Comments