TANESCO MUONGEZE VITUO VYA KUCHAJIA VYOMBO VYA USAFIRI VINAVYOTUMIA UMEME – WAZIRI RIDHIWANI

 


NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amelitaka Shirika la umeme Tanzania ( TANESCO) kuongeza vituo vya kuchajia vyombo vya usafiri vinavyotumia nishati ya  umeme ili kuongeza wigo wa utoaji huduma hiyo ambayo imeonekana kuleta mageuzi katika matumizi ya nishati safi.


Mhe. Ridhiwani ameyasema hayo Juni 17, 2026 alipotembelea Banda la TANESCO katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Chinangali Mkoani Dodoma.


Waziri huyo mwenye dhamana ya Utumishi ametumia nafasi hiyo kuipongeza TANESCO kwa kuendelea kuhamasisha matumizi ya Nishati safi kwa ajili ya  kupikia na katika vyombo vya usafiri.


‘’ TANESCO mnafanya kazi kubwa nawapongeza kwa mageuzi ya matumizi ya nishati ya umeme katika vyombo vya usafiri, natoa rai muongeze Vituo vya kuchajia vyombo hivyo ili kuongeza wigo wa utoaji huduma,’’ alisisitiza Mhe. Ridhiwani


Naye Meneja Masoko Bw. Fredrick Kalinga amesema TANESCO inashiriki katika Maonesho hayo ili kutoa elimu kwa wananchi juu ya huduma na bidhaa zinazotolewa na Shirika ikiwemo maendeleo ya miradi ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji umeme, maboresho makubwa yaliyofanywa na Shirika kwenye mifumo ya kidigitali ya utoaji huduma kwa wateja pamoja na kuhamasisha jamii kutumia nishati safi ya umeme kupikia na katika vyombo vya usafiri kama magari, bajaji, guta, na pikipiki.


Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2026  yenye kauli mbiu isemayo ‘’Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa huduma Endelevu’’ yameanza rasmi Juni 16, 2026 na yanatarajiwa kuhitimishwa Juni 23, 2026.






Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA

UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MSALATO DODOMA KUANZA KUTUMIKA SEPTEMBA 2026

Wasifu wa Kizza Besigye

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA