NA MWANDISHI WETU
WADAU mbalimbali waliotembelea Banda la Wakala wa Vipimo (WMA) katika siku ya kwanza ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Juni 16, 2026 wamekiri kuvutiwa na elimu inayotolewa na timu ya wataalamu kuhusu matumizi sahihi ya vipimo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Nadhifa Nyoni kutoka Mamlaka ya Maji (TANGA UWASA), Rose Mmary (JWTZ) na Janeth Matara, mwananchi mkazi wa Dodoma, wamepongeza kazi zinazofanywa na WMA na kukiri kuwa elimu waliyoipata kutoka kwa wataalamu imewaongezea uelewa kuhusu vipimo.
Kwa upande wake, Abbas Kayanda, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, pamoja na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na WMA, ameshauri kuongeza nguvu katika utoaji elimu ya vipimo ili kuwapatia uelewa wananchi wengi zaidi hususan walioko vijijini.
Ufunguzi rasmi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2026 yaliyoanza leo, Juni 16 katika uwanja wa Chinangali Dodoma, yatahitimishwa Juni 23.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni "Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Maendeleo Endelevu."



Comments