KATIBU MKUU CCM AZUNGUMZA NA WABUNGE WA EALA TANZANIA.

DODOMA | 24 Julai 2026

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amekutana na Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) kutoka Tanzania Makao Makuu ya CCM, Dodoma, na kuwapongeza kwa dhamana ya kuiwakilisha nchi katika chombo hicho cha kikanda.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo Julai 24,2026, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro,amewahimiza kuendelea kutanguliza maslahi ya Taifa na Jumuiya kwa kudumisha mshikamano, kujenga ushirikiano na wabunge kutoka nchi wanachama katika kuimarisha mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao Tanzania inajivunia kuwa moja wa waasisi wake. 

Katibu Mkuu amesisitiza kuwa Chama kina matarajio makubwa kwao na kitaendelea kuwapa ushirikiano wanapotekeleza wajibu wao wa kitaifa na kikanda.






 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

OWM–TAMISEMI YASHINDA TUZO YA MABADILIKO YA KIDIJITALI KATIKA TEHAMA AWARDS 2026

NI MAKOSA WANAFUNZI KUFIKA SHULE SAA 1:15 ASUBUHI

MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU

VIONGOZI NA WATENDAJI WA MATAWI UVCCM PANGANI WANOLEWA

NMB YAWAUNGANISHA WANANCHI NA HUDUMA, FURSA ZANZIBAR