DKT. MDAKU AWAWEZESHA VIJANA KUFIKIA NDOTO ZAO



Ndoto za vijana kutoka Jimbo la Malinyi za kupata elimu ya ufundi na kujijengea maisha bora zimeanza kutimia baada ya kuripoti rasmi katika Chuo cha Victory kilichopo Morogoro kwa ajili ya kuanza masomo yao, wakieleza kuwa fursa hiyo imepatikana kupitia jitihada za Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Mhe. Dkt. Mecktridis Mdaku.


Wakizungumza mara baada ya kuwasili chuoni hapo, wanafunzi hao  wamesema kuwa wamepata matumaini mapya ya maisha kupitia fursa ya elimu itakayowawezesha kupata ujuzi, kujiajiri na kushindana katika soko la ajira.


Wameongeza kuwa, kabla ya fursa hiyo walikuwa hawana uhakika wa kuendelea na masomo kutokana na changamoto mbalimbali, lakini kupitia maono na juhudi za Mhe. Dkt. Mecktridis Mdaku, sasa wameanza safari mpya yenye matumaini makubwa ya mafanikio.


"Tunamshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa kutuamini na kutupa nafasi hii. Tumeahidi kusoma kwa bidii ili kurejea Malinyi tukiwa wataalamu watakaoshiriki kuleta maendeleo katika jamii yetu," alisema mmoja wa wanafunzi hao.


Kwa upande wake, Mhe. Dkt. Mecktridis Mdaku ameendelea kusisitiza kuwa uwekezaji katika elimu na ujuzi kwa vijana ni msingi wa kujenga taifa lenye nguvu kiuchumi, akiamini kuwa vijana wa Malinyi wakipata fursa sahihi watakuwa nguzo muhimu ya maendeleo ya jimbo na Taifa kwa ujumla.


Hatua hiyo ni sehemu ya dhamira yake ya kuendelea kuwawezesha vijana wa Malinyi kwa kuwafungulia milango ya elimu, mafunzo ya ufundi na fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi, ili wawe wazalishaji wa ajira badala ya watafuta ajira.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Soma Taarifa ya UTEUZI:Rais Jakaya Kikwete amemteua Dkt. Ben E. Moshi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya PUMA Energy (zamani ilijulikana kama BP Ltd)

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MAAFISA JENERALI WASTAAFU 17 WA JWTZ WAAGWA.

BINTI WA KITANZANIA GLORIA MAJULE ASHINDA TUZO YA UANDISHI BORA WA FILAMU YA MALARIA MAREKANI ‎

HII NDIYO CV YA KOCHA MPYA WA YANGA

CDF MKUNDA AWATAKA MAAFISA JENERALI WASTAAFU KUACHA KUHANGAIKA NA SIASA

KOCHA WA MC ALGERS AIHOFIA YANGA

MAMBO 16 USIYOYAJUA KUHUSU RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA KIKWETE

VIONGOZI NA WATENDAJI WA MATAWI UVCCM PANGANI WANOLEWA