DSE YAZINDUA HUDUMA UUZAJI, UNUNUZI HISA KIDIGITAL KUPITIA NBC KIGANJANI


NA MWANDISHI WETU

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC Tanzania), kwa kushirikiana na Dar es Salaam Stock Exchange (DSE), imezindua huduma mpya ya ununuzi na uuzaji wa hisa kwa njia ya kidijitali kupitia NBC Kiganjani.


Huduma hiyo inawawezesha Watanzania kununua na kuuza hisa za kampuni zilizoorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa kutumia simu zao za mkononi, bila kulazimika kufika katika matawi ya benki au taasisi za masoko ya mitaji.


Huduma hiyo imeunganisha DSE Hisa Kiganjani na NBC Kiganjani, hatua inayolenga kufanya uwekezaji katika masoko ya mitaji kuwa rahisi na kupatikana kwa watu wengi zaidi.


Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi, amesema huduma hiyo itawawezesha wateja kununua na kuuza hisa, kupata taarifa za soko pamoja na kufuatilia uwekezaji wao kwa urahisi na kwa usalama.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa DSE, Peter Nalitolela, amesema huduma hiyo pia inapatikana kwa watu ambao si wateja wa NBC. Wanaweza kupakua NBC Kiganjani na kufungua akaunti kwa kutumia kitambulisho chao cha NIDA.


Ushirikiano huo ni hatua muhimu katika kuongeza ushiriki wa wananchi katika masoko ya mitaji nchini Tanzania, pamoja na kuhamasisha Watanzania kutumia akaunti zao za benki si kwa ajili ya kuweka akiba pekee, bali pia kujenga utajiri kupitia uwekezaji.


Mkurugenzi wa Utafiti, Sera na Mipango wa CMSA, Alfred Mkombo, ameupongeza mpango huo akisema kuunganishwa kwa huduma hizo kutasaidia kuwafikia na kuwahusisha watu wengi zaidi katika masoko ya mitaji na dhamana kupitia majukwaa ya kidijitali.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

OWM–TAMISEMI YASHINDA TUZO YA MABADILIKO YA KIDIJITALI KATIKA TEHAMA AWARDS 2026

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA KUAPISHWA NDEJEMBI KUWA MAKAMU WA RAIS

NI MAKOSA WANAFUNZI KUFIKA SHULE SAA 1:15 ASUBUHI

MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU

URUSI, CHINA, IRANI NA KOREA KASKAZINI WAPANGA KUUNDA JESHI MOJA LA KUJIHAMI

NDEJEMBI KUTOKA MFANYAKAZI WA GSM HADI KUWA MAKAMU WA RAIS