POLISI YAKAMATA 11 WAKIHUSISHWA WIZI MIUNDOMBINU YA TTCL DAR

 


NA MWANDISHI WETU


KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, amesema wanawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kuiba miundombinu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).


Katika ukamataji wa watuhumiwa hao inadaiwa walipanga njama na kutekeleza uhalifu huo wakiongozwa na Timothy Eshemo maarufu kwa jina la “Jack” wakijifanya kuwa ni Wafanyakazi wa TTCL wakiwa na sululu na msumeno wa kukatia nyaya hizo baada ya kuzifukua.

SACP Muliro amebainisha hayo leo, jijini Dar es Salaam alipozungumza na Waandishi wa habari na kuongeza wataendelea oparesheni hiyo iliyoanza Juni mwaka huu ili kuhakikisha miundombinu ya TTCL inakuwa salama kwa maslahi ya taifa.


 Amefafanua kwamba miundombinu inayodaiwa kuibwa ni pamoja na nyaya za shaba (copper cables), ambazo uharibifu au wizi wake umekuwa ukisababisha kukatika na kuathiri huduma za mawasiliano katika taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi.

"Baadhi ya watuhumiwa walitumia mbinu ya kujifanya kuwa ni wafanyakazi wa TTCL ili kupata fursa ya kufikia miundombinu hiyo na kuiba nyaya zenye shaba, kuanzia sasa mafundi wote watakaokuwa kwenye shughuli yoyote ile kwenye mitaa lazima wakajitambilishe Ofisi ya Serikali iliyo karibu," amesema.

Ameongeza kuwa matukio hayo yalitokea katika maeneo ya Kinondoni, Upanga na Mikocheni, ambapo watuhumiwa hao wanadaiwa kuongozwa na Timothy Eshemo maarufu kama “Jack”.

Aidha amesisitiza wataendelea na uchunguzi ili kubaini mtandao mzima wa watu wanaodaiwa kuhusika na wizi huo na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wote watakaobainika kuhusika.





Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

OWM–TAMISEMI YASHINDA TUZO YA MABADILIKO YA KIDIJITALI KATIKA TEHAMA AWARDS 2026

NI MAKOSA WANAFUNZI KUFIKA SHULE SAA 1:15 ASUBUHI

MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU

VIONGOZI NA WATENDAJI WA MATAWI UVCCM PANGANI WANOLEWA

NMB YAWAUNGANISHA WANANCHI NA HUDUMA, FURSA ZANZIBAR