Na Victor Masangu,Pwani
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa mradi mkubwa wa kimkakati wa Bwawa la kuzalisha umeme wa maji la Mwalimu Julias Nyerere lililopo kata ya Mloka Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani siku Agosti 22 mwaka huu.
Akizungumuza na waandishi habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge amesema kwamba kituo hicho cha kina uwezo wa kuzalisha megawati za umeme zipatazo elfu 2,115 kupitia mitambo tisa iliyokamilika na kuunganishwa na gridi ya Taifa na kwamba kwamba maandalizi yote yanakwenda vizuri.
Aidha katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amesema kwamba serikali imejipanga vilivyo katika suala zima la ulinzi na usalama na kuwahimiza wananchi kuhakikisha wanalinda vyanzo vya maji ikiwemo mradi wa Bwawa hilo ambalo ni mkombozi mkubwa katika kuleta chachu ya kiuchumi na maendeleo kwa wanannchi wa maeneo mbali mbali.
Rais Samia atazindua Bwawa hilo huku mataifa makubwa duniani yakipigwa na butwaa kwa namna ambavyo Tanzania imeweza kukamilisha Bwawa hilo chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Bwawa la kufua Umeme la Mwalimu Nyerere (JNHPP) ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya Tanzania kwa kutumia fedha zake za ndani kiasi cha Sh.Trilioni 7.452 ambapo ujenzi wake ulianzishwa na Rais wa awamu ya tano Hayyat John Pombe Magufuli.
Kukamilika kwa mradi wa kuzalisha umeme wa Bwawa la Mwalimu Julias Nyerere lililopo Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani utaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa nchi nzima kupitia gridi ya Taifa ikiwemo baadhi ya Mikoa ya Pwani, Morogoro, Dar es Salaam, Mkoa wa Lindi pamoja na mikoa mingine
.


Comments