BARABARA YA MAKAMBAKO - SONGEA IMECHAKAA SANA, UKARABATI UTAANZA LINI? - MWANYIKA

Mbunge wa Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika amezidi kuibana Serikali bungeni Dodoma Septemba 4, 2026 kwamba inachukua hatua gani za haraka kuwaondolea Wananchi kero inayotokana na kutumia barabara ya Makambako – Songea ambayo imechakaa? NAIBU WAZIRI WA UJENZI, Godfrey Kasekenya amejibu akama ifuatavyo; Mheshimiwa Spika, Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Makambako – Songea (km 295) umekamilika. Ukarabati wa barabara hii unafanyika kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha ambapo kwa sasa kazi zinaendelea kwa sehemu ya Songea – Lutukira (km 95). Kwa sehemu zilizobaki za Lutukira – Lwangu (km 100) na Lwangu – Makambako (km 100), Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ukarabati.







 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

OWM–TAMISEMI YASHINDA TUZO YA MABADILIKO YA KIDIJITALI KATIKA TEHAMA AWARDS 2026

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA KUAPISHWA NDEJEMBI KUWA MAKAMU WA RAIS

NI MAKOSA WANAFUNZI KUFIKA SHULE SAA 1:15 ASUBUHI

MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU

URUSI, CHINA, IRANI NA KOREA KASKAZINI WAPANGA KUUNDA JESHI MOJA LA KUJIHAMI

PANYA MAGAWA WA SUA TANZANIA AJENGEWA MNARA WA HESHIMA CAMBODIA