DKT. MECKTRIDIS MDAKU ASHIRIKI MAFUNZO YA KIMATAIFA YA USIMAMIZI WA MAJI CHINA

Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Mhe. Dkt. Mecktridis F. Mdaku, ameshiriki mafunzo ya kimataifa yanayolenga kuimarisha usimamizi wa rasilimali za maji, uhifadhi wa udongo na mabwawa, yanayofanyika nchini China.

Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kupitia Wizara ya Biashara, yakiwakutanisha viongozi na wataalamu kutoka mataifa mbalimbali kujifunza mbinu za kisasa za kudhibiti mafuriko, mmomonyoko wa udongo na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza wakati wa ushiriki mafunzo hayo, Mhe. Dkt. Mdaku alisema maarifa anayoyapata yatachangia kuimarisha juhudi za Tanzania katika usimamizi endelevu wa rasilimali za maji na maendeleo ya jamii.

"China imeonesha namna ambavyo teknolojia, mipango madhubuti na usimamizi wa kisayansi vinaweza kulinda vyanzo vya maji na kupunguza athari za mafuriko. Uzoefu huu ni muhimu kwa Tanzania, hususan katika kuimarisha usalama wa maji kwa wananchi,” amesema Dkt. Mdaku.

Ameongeza kuwa ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya maji unafungua fursa ya kubadilishana uzoefu na kutumia mbinu bora zinazoweza kuboresha huduma za maji na kuhifadhi mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Mafunzo hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Taasisi ya China ya Rasilimali za Maji na UNESCO, yakijikita katika usimamizi wa mabonde ya mito, uhifadhi wa udongo na kuongeza uwezo wa miundombinu ya maji kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.







 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA KUAPISHWA NDEJEMBI KUWA MAKAMU WA RAIS

MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU

𝐌𝐉𝐔𝐄 𝐊𝐀𝐂𝐇𝐄𝐑𝐎 𝐌𝐙𝐄𝐍𝐀

URUSI, CHINA, IRANI NA KOREA KASKAZINI WAPANGA KUUNDA JESHI MOJA LA KUJIHAMI

NI MAKOSA WANAFUNZI KUFIKA SHULE SAA 1:15 ASUBUHI

PANYA MAGAWA WA SUA TANZANIA AJENGEWA MNARA WA HESHIMA CAMBODIA