IDARA YA UTAFITI, MIPANGO NA UWEKEZAJI TANESCO WAASWA KUFANYA KAZI KWA UBUNIFU


NA MWANDISHI WETU, MWANZA

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeitaka Idara ya Utafiti, Mipango na Uwekezaji (PRI) kuongeza kasi katika utekelezaji wa mipango na miradi ya kimkakati, likisisitiza matumizi ya teknolojia, wataalamu wa ndani na uzingatiaji wa muda na mikataba ili kuongeza ufanisi wa katika utelelezaji wa miradi 


Wito huo umetolewa Septemba 17, 2026 na Meneja wa TANESCO Mkoa wa Geita, Mhandisi Jahulula Jahulula, akimuwakilisha Mkurugenzi wa TANESCO Kanda ya Ziwa wakati akifunga Kikao Kazi cha Idara ya Utafiti, Mipango na Uwekezaji (PRI Forum), kilichofanyika kwa siku nne katika Ukumbi wa Rockcity Jijini Mwanza.


“Idara yenu ni injini ya TANESCO, kwa kuwa mipango ya miradi mikubwa ya uzalishaji na usafirishaji wa umeme, utafiti na uwekezaji inaanzia katika kazi zinazofanywa na idara yenu, hivyo mafanikio yake yana nafasi kubwa katika kuipeleka TANESCO na Taifa katika hatua za juu zaidi”. Amesema Mha.Jahulula 


Aidha, Amepongeza watumishi wa idara PRI  kwa mchango wao katika utekelezaji na ukamilishaji wa miradi mbalimbali  ya kimkakati,ikiwemo Bwawa la Umeme la Mwalimu Julius Nyerere(JNHPP)lenye uwezo wa megawati 2,115, Mradi wa Umeme wa jua  wa Kishapu, njia ya kusafirisha umeme kutoka Chalinze hadi Dodoma,  kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wa njia ya ya kusafirisha umeme ya kilovoti 220 kutoka Mpomvu hadi mgodi wa GGM.


Amesema kupitia PRI, TANESCO pia inaendelea na miradi ya usafirishaji wa umeme wa kikanda, ikiwemo Tanzania-Zambia Interconnector (TAZA), huku maandalizi ya kuunganisha mifumo ya umeme ya Tanzania na Malawi, Msumbiji, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yakiendelea.


“Kila mmoja wetu sasa anapaswa kufahamu kuwa Shirika linamtegemea na nchi inamtegemea. Endeleeni kuchapa kazi kwa bidii, uzalendo na uadilifu,” animalize Mhandisi Jahulula.





Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA KUAPISHWA NDEJEMBI KUWA MAKAMU WA RAIS

MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU

𝐌𝐉𝐔𝐄 𝐊𝐀𝐂𝐇𝐄𝐑𝐎 𝐌𝐙𝐄𝐍𝐀

URUSI, CHINA, IRANI NA KOREA KASKAZINI WAPANGA KUUNDA JESHI MOJA LA KUJIHAMI

NI MAKOSA WANAFUNZI KUFIKA SHULE SAA 1:15 ASUBUHI

PANYA MAGAWA WA SUA TANZANIA AJENGEWA MNARA WA HESHIMA CAMBODIA