KITUO KIKUBWA CHA KUSAFISHA MAFUTA GHAFI KUJENGWA NCHINI TANZANIA


NA MWANDISHI WETU

SERIKALI ya Tanzania na Uganda zinatarajia  kujenga Kituo Kikubwa cha Kusafisha Mafuta Ghafi katika Mkoa wa Tanga  nchini Tanzania na kuifanya Tanga kuwa kitovu cha Nishati (Energy Hub).


Hayo yameelezwa na Rais wa Uganda,  Yoweri  Kabuta Museveni wakati wa uzinduzi wa matanki ya kuhifadhi mafuta  nchini Uganda uliofanyika tarehe 17 Septemba 2026 , katika mji wa Kampala nchini Uganda  ambapo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta  wa Tanzania, Dkt James Mataragio, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC)  Mussa Makame na Kamishina wa Mafuta Wizara ya Nishati  Godluck Shirima walialikwa.



Museveni amesema mradi huo ni ushirikiano baina ya nchi hizo mbili ambapo hatua hiyo ni kuimarisha usalama wa mafuta katika Ukanda wa Afrika Mashariki, hususani Tanzania na Uganda ambapo mafuta hayo yatatoka nchini Uganda na mengine kutoka nchi zinazozalisha mafuta ya aina hiyo.



Museveni amebainisha kuwa mbali na kituo hicho kikubwa kujengwa Tanzania pia kutajengwa kituo kidogo cha kusafisha mafuta  nchini Uganda.


 

Kwa upande wake  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta  wa Tanzania, Dkt James Mataragio, amesema kuwa kujengwa kwa kitovu cha Nishati mkoani Tanga  ni fursa kwa Tanzania kujitangaza , kuhamasisha  na kuchochea maendeleo katika nchi za Kusini mwa Afrika( SADIC).


Vilevile amesema uwekezaji wa miradi hiyo mikubwa ya mafuta nchini Tanzania, ni kuhamasisha usalama wa upatikanaji wa bidhaa za mafuta katika nchi za kusini mwa Afrika (SADIC).



Ikumbukwe kuwa  nchi hizo mbili  kwa sasa zinatekeleza mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka eneo la Hoima nchini Uganda hadi Tanga katika eneo la  Chongoleani(ECOAP) ambapo utekelezaji wake umefikia 92% na Desemba mwaka huu utakamilika na  mafuta kuanza kusafirishwa katika mabomba husika.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA KUAPISHWA NDEJEMBI KUWA MAKAMU WA RAIS

MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU

๐Œ๐‰๐”๐„ ๐Š๐€๐‚๐‡๐„๐‘๐Ž ๐Œ๐™๐„๐๐€

URUSI, CHINA, IRANI NA KOREA KASKAZINI WAPANGA KUUNDA JESHI MOJA LA KUJIHAMI

NI MAKOSA WANAFUNZI KUFIKA SHULE SAA 1:15 ASUBUHI

PANYA MAGAWA WA SUA TANZANIA AJENGEWA MNARA WA HESHIMA CAMBODIA