LAPORTA AMPA RAIS SAMIA SALAMU ZA POLE KUFUATIA KIFO CHA MWENZAWAKE

Rais wa FC Barcelona, Joan Laporta, ametoa salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mwenza wake, Mzee Hafidh Ameir Hassan, kilichotokea Septemba 7, 2026.


Salamu hizo zimewasilishwa kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, ambaye yuko nchini Hispania kwa ziara maalum ya siku nne katika FC Barcelona kwa mwaliko wa Rais Laporta.

Laporta amekabidhi barua maalum ya rambirambi, akimtaka Rais Samia kuwa na subira, moyo wa ujasiri na nguvu katika kipindi hiki cha majonzi.

Ziara ya Makonda pia inalenga kujadili fursa za ushirikiano kati ya Tanzania na Barcelona katika ukuaji wa vipaji, maendeleo ya kiufundi na maandalizi ya AFCON 2027.

Barcelona inatambulika duniani kwa mfumo wake wa kukuza na kuendeleza vipaji vya wachezaji, jambo linaloifanya kuwa miongoni mwa klabu zinazotumika
kama mfano katika maendeleo ya soka la kisasa. Aidha, sehemu kubwa ya wachezaji wa timu ya taifa ya Hispania iliyotwaa Kombe la Dunia 2026 wametokea FC Barcelona.






 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA KUAPISHWA NDEJEMBI KUWA MAKAMU WA RAIS

MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU

𝐌𝐉𝐔𝐄 𝐊𝐀𝐂𝐇𝐄𝐑𝐎 𝐌𝐙𝐄𝐍𝐀

URUSI, CHINA, IRANI NA KOREA KASKAZINI WAPANGA KUUNDA JESHI MOJA LA KUJIHAMI

NI MAKOSA WANAFUNZI KUFIKA SHULE SAA 1:15 ASUBUHI

PANYA MAGAWA WA SUA TANZANIA AJENGEWA MNARA WA HESHIMA CAMBODIA