NA MWANDISHI WETU
MAKAMISHNA wasaidizi waandamizi wa Uhifadhi wanawake kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wapo nchini Indonesia kushiriki mkutano wa mtandao wa wanawake maafisa waandamizi wa Polisi na vyombo vya vingine vya usalama unaofanyika nchini humo.
Wakiongozwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi -Rasilimali watu na Utawsla Salma Chisonga makamishna hao wanatarajia kutoa uzoefu wao katika masuala ya ulinzi, uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii.
Mkutano huo wa siku tano unawaweka pamoja wanawake kutoka vyombo vya usalama wa nchi mbalimbali duniani kujadili fursa na changamoto katika vyombo vya usalama na vinavyolinda rasilimali za nchi.

Comments