MHANDO AZIDI KUIBANA SERIKALI UJENZI WA OFISI YA MADINI KILINDI



Mbunge wa Kilindi Salehe Mhando ameihoji Serikali bungeni Dodoma Septemba 4, 2026 kwamba ina mkakati gani wa kujenga Ofisi ya Madini Wilayani Kilindi.

WAZIRI WA MADINI ANTHONY MAVUNDE AMEJIBU KAMA IFUATAVYO; Mheshimiwa Spika, Napenda kukutaarifu kwamba, Wizara ya Madini ina jumla ya Ofisi 30 zilizopo katika Mikoa ya Kimadini Tanzania Bara. Wizara itaendelea kuongeza Ofisi katika maeneo mengine pindi itakapojiridhisha eneo husika kumeongezeka shughuli za kimadini kwa kiasi kikubwa na hakuna Ofisi ya Madini iliyo karibu ambayo inaweza kutoa huduma katika eneo hilo. Kwa sasa, Wilaya ya Kilindi inahudumiwa na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Tanga.IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

OWM–TAMISEMI YASHINDA TUZO YA MABADILIKO YA KIDIJITALI KATIKA TEHAMA AWARDS 2026

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA KUAPISHWA NDEJEMBI KUWA MAKAMU WA RAIS

NI MAKOSA WANAFUNZI KUFIKA SHULE SAA 1:15 ASUBUHI

MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU

URUSI, CHINA, IRANI NA KOREA KASKAZINI WAPANGA KUUNDA JESHI MOJA LA KUJIHAMI

PANYA MAGAWA WA SUA TANZANIA AJENGEWA MNARA WA HESHIMA CAMBODIA