Mvua kubwa zinazohusishwa na El Niño sababu yake kubwa huanzia kwenye mabadiliko ya joto la maji katika Bahari ya Pasifiki.
Hali hii hutokea pale ambapo maji ya juu ya bahari katika Pasifiki ya kati na ya mashariki yanapokuwa na joto kali zaidi kuliko kawaida.
Maji hayo yanapokuwa na joto, uvukizwaji huongezeka, na kusababisha hewa yenye unyevu nyevu mwingi kupanda angani. Hewa hiyo inapopoa, hutengeneza mawingu mengi na kuongeza uwezekano wa mvua.
El Niño pia hubadilisha mifumo ya kawaida ya upepo na mzunguko wa hewa unaojulikana kama Walker circulation. Mabadiliko haya huathiri namna unyevunyevu na mawingu yanavyosambazwa katika maeneo mbalimbali duniani.
Kwa sababu angahewa ya dunia imeunganishwa, mabadiliko yanayotokea katika bahari ya Pasifiki yanaweza kusababisha mabadiliko ya mifumo ya mvua katika maeneo yaliyo mbali sana, ikiwemo Afrika Mashariki.
Nchini Tanzania na katika baadhi ya maeneo ya Afrika Mashariki, El Niño inaweza kuhusishwa katika hali ya mvua nyingi kuliko kawaida, haswa katika vipindi fulani vya msimu wa mvua.
Hata hivyo, athari zake hazifanani kila mahali na hutegemea pia hali nyingine za bahari na angahewa.
• Kwa kifupi, El Niño si mvua yenyewe, bali ni mabadiliko makubwa ya joto la bahari na mifumo ya anga ambayo inawesaa kubadilisha mwenendo wa mvua katika sehemu mbalimbali za dunia.
#AstronomyKiswahili

Comments