NAIBU WAZIRI MAHUNDI AMFARIJI RAIS SAMIA

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, ambaye pia ni Mbunge anayewakilisha Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Mbeya, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, Septemba 8, 2026, amekutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, nyumbani kwake Kizimkazi, Zanzibar, na kumpa pole kufuatia kifo cha Mwenza wake, Mzee Hafidh Ameir Hassan.

Mhe. Maryprisca amemfariji Rais Samia na familia yake kufuatia msiba huo, huku akitoa pole na kuwaombea moyo wa subira, uvumilivu na faraja katika kipindi hiki cha majonzi.

Mzee Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia Septemba 7, 2026, wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mzena na amezikwa siku hiyo hiyo Visiwani Zanzibar.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA KUAPISHWA NDEJEMBI KUWA MAKAMU WA RAIS

MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU

NI MAKOSA WANAFUNZI KUFIKA SHULE SAA 1:15 ASUBUHI

URUSI, CHINA, IRANI NA KOREA KASKAZINI WAPANGA KUUNDA JESHI MOJA LA KUJIHAMI

𝐌𝐉𝐔𝐄 𝐊𝐀𝐂𝐇𝐄𝐑𝐎 𝐌𝐙𝐄𝐍𝐀

PANYA MAGAWA WA SUA TANZANIA AJENGEWA MNARA WA HESHIMA CAMBODIA