TANESCO YATUNUKIWA TUZO KUTAMBUA MCHANGO WA UBUNIFU NA MAENDELEO YA NISHATI


NA MWANDISHI WETU

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limekabidhiwa tuzo ya kwa kutambua mchango wa kipekee katika ubunifu na maendeleo ya sekta ya Nishati nchini  ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa Shirika katika kuendeleza sekta hiyo.


Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO katika hafla ya tuzo za ujenzi wa miundombinu na uchimbaji madini kwa mwaka 2026, iliyofanyika Septemba 4, 2026 jijini Dar es Salaam.


Akikabidhi tuzo hiyo Mkurugenzi wa Usajili wa Wakandarasi Wizara ya Ujenzi Mhandisi Rhoben Nkori kwa Niaba ya Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega amelipongeza Shirika kwa kuendelea kuimalisha upatikanaji wa Umeme katika Maeneo mbalimbali hapa nchini Hali ambayo imekuwa Chachu ya kuchochea Maendeleo katika sekta mbalimbali hapa nchini.


Tuzo hiyo imetolewa na Chama cha Ujenzi na Miundombinu cha Tanzania (CCIT), ikiwa ni utambuzi wa mchango wa TANESCO katika ubunifu na maendeleo ya nishati nchini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

OWM–TAMISEMI YASHINDA TUZO YA MABADILIKO YA KIDIJITALI KATIKA TEHAMA AWARDS 2026

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA KUAPISHWA NDEJEMBI KUWA MAKAMU WA RAIS

MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU

NI MAKOSA WANAFUNZI KUFIKA SHULE SAA 1:15 ASUBUHI

URUSI, CHINA, IRANI NA KOREA KASKAZINI WAPANGA KUUNDA JESHI MOJA LA KUJIHAMI

PANYA MAGAWA WA SUA TANZANIA AJENGEWA MNARA WA HESHIMA CAMBODIA