Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Oktoba 9, 2026, imetunukiwa cheti cha Shukrani kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa kutambua kuendelea kuunga mkono mfuko huo kupitia uanachama na michango.
Aidha, NSSF imemtunuku Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mhe. Mary Pius Chatanda (MCC), cheti cha shukrani kwa kutambua mchango wake katika kuunga mkono mfuko huo na kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizo.
Kutunukiwa kwa vyeti hivyo kunaonesha kuthaminiwa kwa ushirikiano na mchango wa UWT pamoja na Mwenyekiti wake katika kuendeleza hifadhi ya jamii.
Comments