DKT. TULIA ATAJA MAFANIKIO YAKE AKIWA RAIS WA IPU

Rais Mstaafu wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson, ametaja mafanikio matano yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake, yakilenga kuimarisha uwajibikaji, ushiriki wa vijana, usawa wa kijinsia na usalama wa viongozi pamoja na watumishi wa mabunge.


Akizungumza katika hotuba yake ya kufunga Mkutano wa 153 wa IPU, leo Oktoba 9, 2026, jijini Arusha, Dkt. Tulia amesema mafanikio hayo yanajumuisha kuanzishwa kwa kipengele maalumu cha uwajibikaji kinacholenga kuhakikisha maazimio ya umoja huo yanatafsiriwa na kutekelezwa katika ngazi za kitaifa.

Ametaja mafanikio mengine kuwa ni marekebisho ya kanuni na sheria za IPU yaliyoweka rasmi nafasi ya Makamu wa Rais wa umoja huo kuwa Naibu Rais, pamoja na kupunguza umri wa wabunge vijana wanaotambuliwa na IPU hadi chini ya miaka 40, hatua inayolenga kuongeza ushiriki wao katika shughuli za umoja huo.

Aidha, amesema IPU imeweka usawa wa kijinsia kuwa lengo la pamoja, huku uwakilishi wa wanawake katika nafasi husika ukifikia asilimia 39.

Mafanikio ya tano ni kupitishwa kwa sera ya kupinga unyanyasaji inayolenga kulinda wabunge na watumishi wa IPU pamoja na watumishi wa mabunge ya kitaifa wakati wa mikutano ya umoja huo.

Dkt. Tulia amehitimisha hotuba yake kwa kusema kuwa licha ya kumaliza muda wake wa uongozi, ataendelea kuwa balozi wa IPU. 

Amesisitiza kuwa mafanikio yaliyopatikana ni matokeo ya ushirikiano na kwamba juhudi za kuimarisha demokrasia hazina mwisho.







 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

KATIKA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA.

YANGA YAMPOTEZA MAMA FATMA KARUME MWANA YANGA KINDAKI NDAKI

𝐌𝐉𝐔𝐄 𝐊𝐀𝐂𝐇𝐄𝐑𝐎 𝐌𝐙𝐄𝐍𝐀

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA