NMB YAONDOA ADA NMB DIRECT KWA SIKU 90

 Benki ya NMB imeondoa ada za miamala kupitia mfumo wake mpya wa NMB Direct kwa siku 90, kuanzia Oktoba 5 hadi Desemba 31, 2026, hatua inayohusisha malipo ya pamoja, uhamishaji wa fedha ndani na nje ya nchi pamoja na malipo ya bili.

Hatua hiyo ni sehemu ya maboresho matatu yaliyotambulishwa wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026, yakiwamo kuanzishwa kwa dawati maalumu la kuwahudumia wateja wenye ulemavu na huduma ya Self-Reversal kupitia NMB Mkononi App na USSD.

Mkuu wa Kitengo cha Benki kwa Wateja Binafsi wa NMB, Filbert Mponzi, alisema dawati hilo litatoa msaada maalumu kwa wateja wenye ulemavu wa kusikia, kuona na viungo, huku wenye ulemavu wa kusikia wakiwezeshwa kupata huduma kwa video inayotumia lugha ya alama.

Kupitia Self-Reversal, wateja wataweza kuanzisha wenyewe maombi ya kurejesha miamala inayostahili bila kulazimika kupiga simu benki au kufika tawi, hatua inayolenga kuongeza urahisi na uwezo wa mteja kupata huduma kupitia teknolojia.









Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

KATIKA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA.

YANGA YAMPOTEZA MAMA FATMA KARUME MWANA YANGA KINDAKI NDAKI

𝐌𝐉𝐔𝐄 𝐊𝐀𝐂𝐇𝐄𝐑𝐎 𝐌𝐙𝐄𝐍𝐀

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA