ECF-SADC IMESAIDIA KUIMARISHA MIFUMO YA UCHAGUZI - JAJI MWAMBEGELE


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania - Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele amesema ushiriki wa Tanzania katika ECF-SADC tangu kuanzishwa kwake mwaka 1998 umeiwezesha nchi kupata fursa za kujifunza na kubadilishana uzoefu na tume nyingine za uchaguzi katika ukanda huo kwani ushirikiano huo umesaidia kuimarisha mifumo ya uchaguzi na kujenga uwezo wa taasisi za usimamizi wa uchaguzi.

Ameyasema hayo Novemba 23, 2026 wakati ufunguzi Mkutano Mkuu wa 28 wa Jukwaa la Tume za Uchaguzi za Nchi Wanachama wa SADC (ECF-SADC) uliofanywa na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, katika hoteli ya Hyatt Regency - The Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UJUE UKWELI KUHUSU JIJI LA MBEYA (GREEN CITY)

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA

TIMU YA NGORONGORO KAMA DOUMBIA