ELIMU HAIMTUPI MJA WAKE"

 


NA MWANDISHI WETU

Waswahili husema, "Elimu ni bahari", maana yake ni kuwa kuongeza maarifa na ujuzi hakuna kikomo kwa kuwa dunia hubadilika kutokana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.


Uhalisia wa methali hiyo umeonyeshwa na Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Dkt. Abdul-Razaq Badru (PhD) ambae amehitimu rasmi shahada ya udaktari wa Falsafa katika mahafali ya 45 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) yaliyofanyika leo tarehe 27 Novemba, 2026 Bungo Kibaha Mkoani Pwani


Baada ya kutunukiwa Shahada za Uzamivu na Mkuu wa Chuo hicho Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, Dkt Badru ameeleza kuwa kuhitimu shahada hiyo kumemuongezea chachu ya kuendelea kutekeleza kikamilifu majukumu ya Uhifadhi, Utalii na maendeleo ya jamii katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.






Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

TIMU YA NGORONGORO KAMA DOUMBIA

TUCTA WAPATA RAIS MPYA

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA