NA MWANDISHI WETU
MKUU wa Idara ya Menejimenti ya Rasilimali Watu Taaluma Dkt. Judith Msangi akimuwakilisha Mkuu wa Taasisi, akiwa na wahasibu wa #ISW amepokea tuzo ya Uandaaji Bora wa Hesabu za Kifedha chini ya Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu wa Sekta ya Umma (IPSAS), kundi la Vyuo vya Elimu ya Juu, ambapo Chuo cha Ustawi wa Jamii kimeibuka mshindi wa tatu katika uandaaji ya Taarifa za hesabu za mwaka 2025.
Hafla ya utoaji wa tuzo hizo imefanyika Novemba 26, 2026, katika Viwanja vya APC Bunju, Dar es Salaam, ikiwa sehemu ya Mkutano wa 39 wa Wahasibu (39th Accountants' Annual Conterence), uliowakutanisha wahasibu na wadau mbalimbali kutoka taasisi, mashirika, kampuni na sekta binafsi.
Ikumbukwe chuo cha Ustawi wa Jamii kinatwaa tuzo hiyo kwa mara tisa mfululizo tangu mwaka 2017, ishara inayoonyesha juhudi na weledi endelevu wa kuandaa Hesabu na Taarifa za Kifedha.




Comments