KAMBI YA MATIBABU YA KIBINGWA KUANZA NOVEMBA 16 HOSPITALI YA TUMBI

Na Mwandishi wetu, Pwani

Madaktari bingwa kutoka hospitali mbalimbali nchini wanatarajia kutoa huduma za matibabu ya kibingwa na bobezi kwa wananchi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani ya Tumbi, kuanzia Novemba 16 hadi 20, 2026. 

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, amesema kambi hiyo itakuwa maalumu kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani na maeneo jirani kupata huduma za kibingwa bila malipo.

Amesema huduma hizo zitatolewa kwa siku tano, kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni, huku akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo kupata uchunguzi na matibabu kutoka kwa madaktari bingwa.

Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani ya Tumbi, Dk. Silas Msangi, amesema maandalizi ya kambi hiyo yanaendelea vizuri na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kupata huduma hizo.

Ameeleza kuwa madaktari bingwa watakaoshiriki katika kambi hiyo wanatoka mikoa ya Singida, Iringa, Morogoro, Dodoma na Pwani.

Kambi hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa huduma za kibingwa na bobezi kwa wananchi bila gharama yoyote. 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NMB, UDSM waendeleza ushirikiano wa kukuza vipaji

MILIKI UBUNIFU MAJESHINI KULINDWA KISHERIA

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA

UJUE UKWELI KUHUSU JIJI LA MBEYA (GREEN CITY)