KAMISHNA DKT.BADRU ATUA KAMBI YA TIMU YA NGORONGORO KAMA SELEMANI MWALIMU


NA MWANDISHI WETU 


Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro Dkt. Abdul-Razaq Badru jana usiku tarehe 9 Novemba. 2026 alitua kwenye kambi ya timu hiyo inayoshiriki mashindano ya SHIMMUTA mkoani Morogoro kukagua hali ya kambi hiyo na maendeleo ya wachezaji.


Mara baada ya kukutana na wachezaji hao Dkt.Badru ametoa maelekezo ya wanamichezo wa Ngorongoro kutumia fursa hiyo Kama mojawapo ya kujifunza mambo mapya kutoka taasisi nyingine.


“Tumieni michezo kuitangaza Ngorongoro, chezeni kwa nguvu zenu zote Ila mkumbuke michezo ni furaha na amani na muwe tayari kupokea aina yoyote ya matokeo,”alisema Dkt.Badru.


Ofisa Michezo wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Yotham Gitige alimshukuru kamishna kwa ziara hiyo na kusema kuwa imewatia moyo katika ushiriki wao kwenye michezo hiyo.




Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MWENGE WA UHURU WAMURIKA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KWELA

NMB, UDSM waendeleza ushirikiano wa kukuza vipaji

SERIKALI ITAENDEA KUHIMIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KUIMARISHA UTENDAJI KAZI- LONDO

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA