SAMIA AIPA TANZANIA HESHIMA AFRIKA UPUNGUZAJI VIFO VYA MAMA NA MTOTO


NA MAGENDELA MRISHO


TANZANIA imekuwa kivutio kwa mataifa mengine ya Afrika baada ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa kinara katika kupunguza vifo vya mama na mtoto.


Hatua imefanya baadhi ya nchi za Afrika kuiomba Tanzania ikiwemo Ghana kuzipa elimu ya kupunguza vifo na mtoto katika mataifa yao na baadhi ya maifa tayari yameanza kupewa elimu ikiwemo Kenya.


Maombi yamejitokeza wakati Rais Samia alipofanya ziara nchini Ethiopia ambako alizindua mpango wa kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.


Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa amebainisha hayo leo Novemba 24, 2026 akizungumza na Waandishi wa Habari kubainisha mafanikio yaliyopatikana katika mataifa ya Ethiopia na Uganda baada ya Rais Samia kufanya ziara katika mataifa hayo.


  Amesema Tanzania imeweza kufanikiwa  kupunguza vifo vya mama wajawazito, wanawake wakati wa kujifungua na watoto wachanga kupitia uwekezaji katika miundombinu ya afya, huduma za msingi pamoja na kuimarisha upatikanaji wa wataalamu wa afya nchini.


Ameongeza kwamba  katika uzinduzi wa mpango wa Afrika Mashariki wa kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga, uliofanyika nchini Ethiopia uliolenga kuimarisha ushirikiano wa nchi wanachama na Rais w Samia alisisitiza umuhimu wa uongozi wenye dhamira, uwekezaji endelevu na utekelezaji wa hatua zinazotokana na ushahidi ili kuokoa maisha ya mama na watoto.


Katika uzinduzi huo Rais Samia alitoa wito kwa nchi wanachama kuhakikisha ahadi za kisiasa zinabadilishwa kuwa matokeo halisi kwa kuimarisha huduma za afya, kuweka mipango inayotekelezeka na kuhakikisha uwekezaji unaelekezwa katika maeneo yenye mahitaji makubwa" amesema.


Mchengerwa amesema ili mataifa mengine Afrika yafanikiwe  katika hatua hiyo wanatakiwa  kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika ujenzi na upanuzi wa vituo vya afya, zahanati na hospitali za wilaya, ili kusaidia kusogeza huduma karibu na wananchi na kupunguza umbali wa kufuata huduma za afya, hususan kwa wajawazito na watoto ambalo Tanzania imefanya na kufanikiwa kupiga hatua hiyo inayovutia mataifa mengine kuja kujifunza.


Alisema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya karibu na maeneo wanayoishi, huku ujenzi wa miundombinu ukienda sambamba na kuimarisha ubora wa huduma zinazotolewa katika vituo hivyo.


Aidha, mpango huo umejengwa katika maeneo makuu matatu ya kimkakati ambayo ni kuimarisha uongozi wa kisiasa ili afya ya mama na mtoto iwe kipaumbele katika maamuzi ya Serikali, kuhamasisha uwekezaji katika mifumo ya utoaji huduma za afya na kuhakikisha utekelezaji wa hatua zinazotokana na ushahidi wa kitaalamu.


Katika mpango huo, Tanzania imeelezwa kuwa na nafasi muhimu katika kuimarisha huduma za afya ya msingi, ambazo zinahusisha zahanati, vituo vya afya na hospitali za halmashauri, zinazohudumia sehemu kubwa ya wananchi.


Serikali pia imekusudia kuimarisha huduma za uzazi, watoto wachanga, huduma salama za kujifungua, huduma za dharura za uzazi na watoto wachanga, mifumo ya rufaa pamoja na mafunzo kwa watumishi wa afya ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.


Mpango huo pia unalenga kutoa fursa za mafunzo kwa wataalamu wa afya, hususan vijana, kwa kuanza na nafasi 60 ambazo zitawawezesha kupata ujuzi maalumu katika huduma za afya ya mama, uzazi na watoto wachanga, huku fursa nyingine zikiendelea kuongezwa kulingana na upatikanaji wa rasilimali na ushirikiano wa wadau.


Katika hatua nyingine, Serikali inatarajia kushirikiana na sekta binafsi, wafadhili na washirika wa maendeleo kuongeza uwekezaji katika afya ya mama na mtoto, huku nchi wanachama zikiendelea kuwa na jukumu kuu la kutekeleza mipango hiyo kupitia mifumo yao ya kitaifa ya afya.


Utekelezaji wa mpango huo unatarajiwa kuimarisha ushirikiano wa nchi za Afrika Mashariki, kuongeza uwajibikaji wa viongozi na wataalamu wa afya, pamoja na kuhakikisha hatua zinazochukuliwa zinakuwa na matokeo yanayopimika katika kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika vya mama na watoto wachanga.


Mpango huo unalenga kuwa chachu ya mabadiliko katika sekta ya afya kwa kuweka kipaumbele katika kuokoa maisha, kuimarisha huduma za uzazi na kuhakikisha kila mama na mtoto anapata huduma bora, salama na kwa wakati.


Naye Waziri Uchukuzi, Prof. Makame  Mbalawa akizungumzia mafanikio yaliyofanywa na Rais Samia nchini Uganda amesema wamefanikiwa kusaini makubaliano ya kuindoa vikwazo vya kibiashara vitakavyosaidia wananchi mataifa hayo kuinuia uchumi kupitia Nyanja hiyo na kutoa wito kwa vijana kukimbilia fursa za kibiashara zilizopo Katika nchi hizo.


Aidha aliweka wazi kwamba pia wamekubaliana kujenga reli ya kisasa (SGR) ya urefu wa km 620 ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka Tanzania kwenda Uganda.





Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UJUE UKWELI KUHUSU JIJI LA MBEYA (GREEN CITY)

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA

TIMU YA NGORONGORO KAMA DOUMBIA