KIJANA WA MBEYA AENDELEA KUTOA DOZI YA KUTIBU MAGONJWA SUGU

 Kijana Jafari Wema ama Fikiri akigawa dozi kwa mmoja wa wakazi wa Mbeya waliojitokeza kupata huduma hiyo
Mmoja wa wasaidizi wa Mjukuu wa kiokombe akikokea moto kuchemsha dawa
Na Thompson Mpanji,Mbeya

KIJANA mdogo aliyeibuka na kuanza kutoa huduma ya tiba kwa kutumia kikombe kama alivyokuwa Babu wa Kijiji cha Samunge,Wilaya ya Loliondo,Mch.Ambilikile Mwasapila ameishukuru serikali kwa  kumruhusu kuendelea kutoa huduma  kwa jamii lakini mizimu yake imekataa kufanya huduma hiyo nje ya nyumbani kwao kwani  dawa hiyo haitafanyakazi.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi,kijana Jafari Werna au Fikiri (17) maarufu ‘Babu mtoto wa mabatini,’alisema baada ya kuitwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Bw.John Mwakipesile ofisini kwake alimweleza kuwa yeye ni kijana mdogo hivyo hapaswi kufanya shughuli ya uganga wa jadi hadi atimize  umri wa miaka 18 na zaidi.

Alisema  baada ya kujieleza kuwa shughuli hizo alianza akiwa na umri mdogo kwani alikuwa amerithishwa na Bibi yake hivyo alitakiwa kukata kibali ambacho alilipiwa kiasi cha sh.55,000 baada ya viongozi wake wa mashina (mabalozi) na serikali ya Mtaa  wa Mianzini anapoishi kufanya mchango huo.

“Sasa naendelea kutoa huduma na wakaribisha waje wahitaji kutoka maeneo mbalimbali nje na ndani ya mikoa,nawaambia hasa wagonjwa na wenye shida mbalimbali ziwe za ukimwi na magonjwa sugu wanaoishi ndani ya mkoa wa Mbeya wawahi kwani itafika wakati watapata shida kuniona kabisa,alisema.

Aliongeza,”madudu yangu yamekataa kuhama hapa na yamesema nikihama hapa hii tiba haitafanyakazi tena, wagonjwa na wahitaji waje watu wanapona na wanarudi kunishukuru,wanakunywa kikombe  kimoja leo na kingine kesho basi, wanachangia Sh.200 ya kuni za kuchemshia dawa,na kama wanataka kuniona kwa shida nyingine Sh.1000, viongozi wa shina na mtaa wanaendelea kuboresha huduma na usafi ili kuondokana na magonjwa ya milipuko.”

Mwandishi wa habari hizi amekuta msululu wa magari yaliyoegeshwa katika maeneo mbalimbali ya mtaa wa mianzini huku maelfu ya wananchi katika foleni wakiwa wameshika kikombe cha plastiki mkononi wangine  wakiwa wamebebwa katika  machela na ndugu,jamaa na marafiki.

Akisimulia historia yake Jafari alisema alishindwa kumaliza masomo akiwa kidato cha kwanza mkoani morogoro  baada ya kushindwa kusoma na kutokewa na maruwe ruwe na kushindwa kuona  katika ubao na hivyo kurudishwa nyumbani kwa Bibi yake mzaa mama yake aliyefariki mwaka 2004 mkoani Mbeya ambapo alikabidhiwa mikoba na Bibi yake na kuanza kufanya shughuli za uganga akiwa na umri mdogo.

“Baada ya mama kufariki baba alinichukuwa kwenda morogoro na huko nikashindwa kuendelea na masomo kutokana na kutokewa na vitu vya ajabu na kushindwa kuona,nikarudishwa kwa Bibi na baadaye nilipoanza uganga   siku moja nilioteshwa kuna dawa ya kuponywa  ukimwi na magonjwa sugo Mbozi ingawa mbozi sikujuwi nilichukuliwa na kwenda kuchimba usiku na ndiyo hii ninayotoa tiba,”alisema.

Baadhi ya wananchi waliofika kupata kikombe kwa kijana Jafari wamemshukuru mungu kwa  kuwaletea tabibu huyo ambaye atawasaidia hata watu wasio na uwezo wa kwenda Loliondo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI