TBL YAJENGA KISIMA CHA SH. MIL.9 KITUO CHA AFYA YA UZAZI MBAGALA

Mama Mkazi wa Mbagala, Daima Ahamad aliyejifungulia mtoto katika Kituo cha Mbagala, Round About, akitoa shukrani kwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na Rotary Cub Mikocheni, kwa kuwezesha ujenzi wa kisima cha maji chenye matanki mawili ya kuhifadhiwa lita 10,000 za maji. Kisima hicho ambacho ujenzi wake uligharimu sh. Mil. 9 zilizotolewa na TBL kilikabidhiwa kwa uongozi wa kituo hicho juzi.

Wanachama wa Rotary Club Mikocheni, wakiongozwa na Rais wao, Irene Kamau ( wa pili kulia) wakimshukuru Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kushoto), baada ya ya kukabidhi kwa Kituo cha Afya ya Uzazi cha Mbagala Round About, Temeke Dar es Salaam juzi, mradi wa kisima cha maji chenye matanki mawili ya kuhifadhia lita 10,000 kilichojengwa kwa ufadhili wa TBL kwa gharama ya sh. Milioni 9. (Wapili ushoto ni, Daktari Mkuu Mfawidhi wa kituo hicho, Batuli Luhanda.

Rais wa Rotary Club Mikocheni, Irene Kamau (kulia) na Daktari Mkuu Mfawidhi wa Afya ya Uzazi cha Mbagala Round Abaout, Batuli Luhanda ( wa pili kulia), wakimshukuru Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kushoto), baada ya kukabidhi kwa kituo hicho, mradi wa kisima cha maji chenye matanki mawili ya kuhifadhia lita 10,000 kilichojengwa kwa ufadhili wa TBL kwa gharama y ash. Milioni 9.


Daktari Mkuu Mfawidhi wa Kituo cha Afya ya Uzazi cha Mbagala Round About, Temeke, Dar es Salaam, Dk. Batuli Luhanda (kushoto), akitoa shukrani kwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na Rotary Club Mikocheni kwa kuwezesha ujenzi wa kisima cha maji chenye matanki mawili ya kuhifadhia lita 10,000 za maji katika kituo hicho. Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu aliyekabidhi kisima hicho juzi, kilichojengwa kwa gharama ya sh. Milioni 9

Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kulia) na Rais wa Rotary Club Mikocheni, Irene Kamau wakikata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi kisima cha maji chenya matanki mawili ya kuhifadhi lita 10,000 za maji kwa Kituo cha Afya ya Uzazi cha Mbagala Round About, Temeke, Dar es Salaam juzi. Anayeshuhudia kushoto ni Daktari Mkuu Mfawidhi wa kituo hicho, Batuli Luhanda. Kupitia Rotary hiyo TBL ilifadhili mradi huo kwa gharama y ash. Milioni 9.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

TOFAUTI YA WATU WA DAR NA WA MKOANI NI HUU

IBENGE: YANGA SC WATAFUZU HATUA YA ROBO FAINALI.

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA