JESHI KENYA LAZIMA SHAMBULIO AL-SHABAAB



Msafara Serikali ya mpito ya Somalia imesema vikosi vyake vinavyosaidiwa na majeshi ya Kenya, vimefanikiwa kuzima shambulio la wapiganaji wa al-Shabaab.

Msemaji wa vikosi vya Somalia ameiambia BBC kuwa wamewaua wapiganaji 36 wa al-Shabaab walipopambana eneo la kusini.

Lakini kamanda wa al-Shabab amesema wanamgambo hao wameharibu magari ya kijeshi ya Kenya na kusababisha majeruhi wengi.

Majeshi ya Kenya ambayo yaliingia Somalia mwezi uliopita, yametahadharisha kutoke kwa mashambulizi kwenye miji kumi nchini Somalia kwa kupitia mtandao wa jamii Twitter.

Kenya inawalaumu wapiganaji wa al-Shabab kwa matukio ya utekaji nyara wageni katika ardhi yake.

Lakini kundi hilo lenye uhusiano na al-Qaeada na linadhibiti sehemu kubwa ya kusini mwa Somalia, limekanusha kuhusika.
Shehena ya silaha

Kamanda wa al-Shabab katika eneo hilo Sheik Mohamed Ibrahim alisema msafara wa magari ya kijeshi ya Kenya ulivamiwa kwenye barabara kutoka mpaka wa mji wa Liboi wakati vikosi vya Kenya vikielekea mbele nchini Somalia.

"Wapiganaji wa mujahideen wameharibu magari kadhaa ya kijeshi katika msafara huo," alisema Bw Ibrahim.

Msemaji wa jeshi la Kenya Meja Emmanuel Chirchir, alithibitisha kuwa kumekuwa na mapambano ya moto kati ya Vikosi vya Kenya na watu wanne wanaohofiwa kuwa wapiganaji wa al-Shabaab.

Amesema msafara wake uliwataka watu wanne wenye silaha kusimama lakini wakaafyatua risasi.

"Tunachosema watu wawe makini wasijichanganye na al-Shabab. Huo ndio ujumbe wetu. "

msemaji wa Jeshi la Kenya Meja Emmanuel Chirchir.

Meja Chirchir pia alionya wakazi wa miji kumi kuwa waangalifu na mashambulizi ya anga.

Baadaye alifafanua kupitia BBC kuwa ngome za wapiganaji wa al-Shabab walikuwa nje ya miji hiyo na kwamba walikuwa wanalenga kambi zao.

Ameongeza kuwa ilikuwa ni vigumu kutoa taarifa kama hiyo kupitia Twitter ambayo inaruhusu herufi 140 za ujumbe.

Alisema Kenya ilikuwa ikifuatilia shehena mbili za silaha wanazopelekewa al-Shabab ambazo zimesafirishwa Somalia katika siku mbili zilizopita, na majeshi yake yatashambulia ngome yoyote ya waasi ambako silaha zitawekwa.

Miji tisa iliyotajwa kupitia Twitter ni Baidoa, Bardhere, Dinsor, Afgoye, Buale, Barawe, Jilib, Kismayo and Afmadow.

Aliongeza kuwa maamuzi ya kuanza harakati na mashambulizi yataanza ‘wakati wowote’ kuanzia Jumatano.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

TOFAUTI YA WATU WA DAR NA WA MKOANI NI HUU

IBENGE: YANGA SC WATAFUZU HATUA YA ROBO FAINALI.

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA