TIGO YAZIDI KUMWAGA ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA ZAMU YAKO KUSHINDA

Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Alice Maro (kushoto) akimkabidhi zawadi ya kompuyuta ndogo, Asmah Abdalah katika hafla ya kuwakabidhi washindi wa promosheni ya 'Zamu Yako Kushinda', Dar es Salaam leo. Katikati ni Mratibu wa Promosheni na Matukio wa Tigo, Edward Shila.
Mkazi wa Tabata Segerea, Filbert Lyimo (kulia) akipewa zawadi ya Laptop
Alice Maro akimpatia zawadi ya laptop, Mkazi wa Tabata Segerea, Esther Cheyo


Mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam, Maglani Maleko akikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 4 baada ya kuwa mmoja wa washindi wa promosheni hiyo.
Frank Sekunonga wa Mbezi Beach, Dar es Salaam akikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 4
Mkazi wa Buguruni, Dar es Salaam, Amir Bakar (kulia) akifurahia kupata kompyuta ndogo inayochagiwa kwa kutumia mwanga wa jua (Solar Power)

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Tigo yawazawadia washindi wa promosheni ya “ZAMU YAKO KUSHINDA”

14 Februari, 2012, Dar es Salaam. Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imewazawadia washindi wanne, kila mmoja shilingi milioni nne, (Tsh. 4,000,000/-) kama washindi wa kwanza wa kila siku ambao wamepatikana katika promosheni inayoendelea ya “Zamu yako Kushinda.” Halikadhalika washindi wengine nane wamezawadiwa kompyuta aina ya laptop za Samsung. Washindi wamepatikana katika kipindi cha siku 4.

“Tunapoelekea mwisho wa promosheni hii tungependa tuwashukuru wateja wetu wote walioshiriki,” alisema Alice Maro, Afisa Mahusiano wa Tigo. “Wale ambao hawaja shinda wasikate tamaa bado wana nafasi ya kushinda zimebaki siku 5 tu na promosheni yetu itafikia mwisho,” alisema.

Washindi wa Tsh. 4,000,000/- ni Willy Mtenga (Arusha); Pendo Leverian (Kihonda-Morogoro); Magren Maleko (Mbezi Kimara) na Frank Geoffrey (Mbezi Beach).

Washindi wa laptop ni Asma Abdallah (Magomeni); Esther Cheyo (Tabata Segerea); Liberty Lyimo (Tabata Segerea); Juma Omar Lukengele (Kimara Bonyokwa); Ameir Bakari (Buguruni); Blake Ally Blake (Mwananyamala); Erick Chuma (Tanga) and Rashid Gunde (Ilala Sharif Shamba).

Ili kushiriki mtumiaji wa Tigo anatakiwa kutuma neno “TIGO” kwenda 15571. Gharama kwa kila ujumbe ni Tsh 450. Washiriki wanatakiwa kujikusanyia pointi nyingi ili kujiwekea mazingira mazuri ya kujishindia zawadi. Washiriki pia watazawadiwa zawadi za kutuma ujumbe wa bure kutoka Tigo kwenda mitandao yote Tanzania.

Watumiaji wa mtandao wa Tigo wenye umri chini ya miaka 18, hawaruhusiwi kushiriki. Promosheni hii ni kwa ajili watumiaji wa Tigo watanzania.

Kuhusu Tigo:

Tigo ni mtandao wa simu za mkononi ya kwanza Tanzania, ilianza biashara mwaka 1994 na ni mtandao wa simu Tanzania wenye ubunifu ya hali ya juu na bei nafuu kupita zote nchini. Tigo ni sehemu ya MillicomInternational Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mkononikwa gharama nafuu na inayopatikana maeneo mengikiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanaoibukaAfrika na Amerika ya Kusini.

Msingi wa mafanikio ya Tigo ni uzingatiaji wa mikakati mitatu ambao,ni Gharama nafuu, Uwepo na Upatikanaji .Tunajenga dunia ambapo huduma za simu ni za bei nafuu, zipo na zinapatikana kila mahali na kwa wote. Hii inahakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma bora zaidi kwa bei nafuu kuliko zote katika mikoa yetu 26, Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz

Imetolewa na:

Alice Maro • PR-Tigo • Simu 255 715 554501

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI