Maiti ajali ya Kibaha watambuliwa


MAITI za abiria waliopoteza maisha katika ajali ya mabasi mawili madogo wilayani Kibaha wametambuliwa na baadhi wameanza kuchukuliwa na ndugu zao kwa ajili ya mazishi.

Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, Mkuu wa Upelelezi mkoani humo Evance Mwijage alisema kuwa majeruhi wanne kati ya 42 wamehamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

Mwijage aliwataja marehemu waliotambuliwa kuwa ni James Senga, (49) mkazi wa Mkuza kwa Mfipa ambaye ni fundi mchundo, Hadija Abdulrhaman(25), mkazi wa Miembesaba na mtoto wake wa miaka mitatu na nusu Abdallah Juma.Wengine ni Siwema Ally (28) mkazi wa Tandika Dar es Salaam na mtoto wake Mariam Ally aliyekuwa na umri wa miaka mitatu.

Alisema majeruhi waliohamishiwa MNH hali zao zimebadilika na kuwa mbaya hivyo kuhitaji kupatiwa vipimo na matibabu zaidi.Mganga Mkuu wa Hospitali ya Tumbi, Izaack Lwali amethibitisha kuhamishwa kwa majeruhi hao wanne aliowataja kuwa ni Kelvin Pius (23), mkulima wa eneo la Mwendapole Kibaha, Josephat Lukio (39), mkazi wa Picha ya ndege, Muhsin Sonaga (34), mkazi wa Picha wa ndege na Alex Masawe (27), mkazi wa Mbezi Dar es Salaam.

Dk Lwali alisema majeruhi wengine wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali Teule ya Tumbi ambao ni Majaliwa John, (33), Mwanaharusi Adam (20), Talha Zarau na Mwanahamisi Ally( 29).Wengine ni Saidi Alfa (12), Mussa Fadhili (22), Jonas Nyasika (27) na Anita Iromo (37) wakiwamo pia Amina Zarau (13), Mohamed Twaha (24), John Dastan (31) na Sara Iromo (30).

Athumani Hamisi (2), Amina Rashid (39), Abdallah Dihila, Hamisi Rajabu (19) na Rehema Hamisi (32).Wengine ni Mstapha Adamu – mtoto mdogo, Hidaya Salumu (24), Adamu Ally (63) Beatrice Nyangi (29), Emmanuel Zabron (17) na Magdalena Maiko (26).

Kuruthumu Azizi (21), Salvina Gerald (18), Obadia Mandembwe (44), Jackson Peter (20), Mwajuma Mapunda (15), Iddi Selemani (17) na Masoud Ally (31).

Wametajwa pia Jumanne Ramadhani (36), Hanita Obadia (37), Masoud Masoud (31) Askari JWTZ kikosi cha 36 KJ, Salumu Omari (35), Peter Ndiu (59) pamoja na Halifa Kigomba (50).Ajali hiyo ilitokea Machi 3 katika eneo la Kwa Mbonde Kibaha ikihusisha gari aina ya Toyota Coaster lililoendeshwa na dereva aliyejulikana kwa jina moja la Babu ambaye ni marehemu lililotokea Dar es Salaam kwenda Mlandizi ambapo liligongana uso kwa uso na Isuzu Journey iliyokuwa ikitokea Mlandizi kwenda Dar es Salaam

Afisa habari wa polisi Pwani alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Coaster kuyapita magari mengine kwa mwendo kasi bila kuchukua tahadhari.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*