ZITTO AITAKA SERIKALI IWAJIBIKE KUELEZA KITENDO CHA DK ULIMBOKA KUTEKWA, KUPIGWA

Dr. Ulimboka kutekwa, kupigwa na kuumizwa: Serikali inawajibika kutueleza

Dr. Steven Ulimboka
Ujumbe amenitumia Daktari yupo pale MOI
‘Kaka Zitto,hali ya Dr.Ulimboka yuko unconscious,multiple ribs fracture na kwenye mikono pia amevunjika pamoja na taya,yuko icu wanamstabilise kwanza kwasababu hapumui vizuri,the situation here is really bad,I agree with you this is outright outrageous’
Nimechukizwa sana na habari za kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Dr Ulimboka, Kiongozi wa Madaktari Nchini. Mambo kama haya tumezoea kuyasikia kwenye nchi za kidikteta na kuongozwa kiimla ambapo watawala badala ya kutumia njia ya kidemokrasia na kisheria kushughulikia wanaoamini ni maadui zao katika utawala, hutumia wahuni katika Taasisi za usalama kuteka raia, kuwatesa, kuwafunga na hata kuwaua.

Sitaki kuamini kwamba Tanzania imefikia huko. Nimezungumza na baadhi ya madaktari walio karibu na Dokta Ulimboka na kujulishwa kwamba majeruhi huyu wa vitendo vya hovyo kabisa kutokea hapa nchini alikamatwa jana usiku mnamo saa sita na watu wasiojulikana na kupelekwa katika msitu wa MagwePande na kujeruhiwa vibaya. Habari hizi bado hazijathibitishwa na vyanzo huru lakini ndio zilizopo hadi hivi sasa.

Serikali kama mlinzi wa usalama kwa raia inaWAJIBU kueleza tena kwa haraka ni nini kimetokea kwa kijana huyu msomi na kiongozi wa wataalamu wenzake. Serikali INAWAJIBIKA kueleza katika nyakati kama hizi ambapo kuna mgogoro kati yake na madaktari imekuwa wapi kuhakikisha usalama wa viongozi wa madaktari ili kuepusha watu wanaoitwa ‘agente provocateure‘ kuweza kuhatarisha hali ya amani ya nchi na hata kupelekea kuweka hali ya vitisho kwa madaktari wetu.

Serikali INAWAJIBIKA kueleza kama sasa imeamua kutumia njia za kihuni kumaliza matatizo na wananchi wake.

Nimemuomba Waziri kivuli wa Afya wa CHADEMA kufuatilia suala hili kwa kwa karibu sana ili kuhakikisha kwamba ukweli wote na ukweli mtupu unafahamika. Kamwe hatuwezi kuacha Mtanzania yeyote aonewe, anyanyaswe au akandamizwe eti kwa sababu ya kudai haki yake na za wenzake. ‘An injury to one, injuries to all’
Naomba madaktari wamwangalie kwa karibu daktari mwenzao ili aweze kupata nafuu. Ulinzi uimarishwe ili kuhakikisha usalama wake.

Comments

Anonymous said…
IWAPO MMEGOMA KUWATIBU WATANZANIA, JE MMEGOMA PIA KUWATIBU NDUGU NA JAMAA ZENU?? ULIMBOKA JE?? AU MMEAMUA KUTIBIANA NYIE KWA NYIE?? KWA FEDHA ZA WANANCHI WA KUTOKA WAPI?? VIFAA VYA MUHIMBILI MNAVYOMTIBIA ULIMBOKA MNAJUA NI DAMU NA JASHO LA NANI??

NYINYI MNASHABIKIA DOKTA ULIMBOKA HIVI, DOKTA ULIMBOKA VILE, NA KUHITIMISHA KWA KAULI KWAMBA ATIBIWE VYEMA NA KISHA KUWEKEWA ULIN ZI MAHSUSI, SASA SWALI LANGU NI HILI, KUNA WATANZANIA WANGAPI WAMERIPOTI HOSPITALI MBAI MBALI ZENYE MIGOMO HAPA NCHINI TENA WENGI WAO KWA MAJERAHA YA KUPIGWA KAMA YEYE, UKIZINGATIA ALIYEITISHA MGOMO NDIYE YULE YUE ULIMBOKA, KWANINI NAYEYE ASIACHWE KWANZA HADI MGOMO UISHE ILI FAMILIA YAKE NAYE IONJE KILE AMBACHO FAMILIA ZA WATANZANIA WOTE WANAOUGULIW KUONJA??

AU MGOMO HUU NI WA KUTO KUWATIBU WATANZANIA WA CHINI TUU NA HAUWAHUSU MADAKITARI WENZA????

NA NI KWANINI KILA MTU ANAITOLEA MACHO SEREKALI KUTOKANA NA HILI?? SEREKALI YA TANZANIA INGEKUWA NA TABIA HII, NI VIONGOZI WANGAPI WA KAMBI YA UPINZANI HUIPINGA SERKALI NA TENA KWA KUTOLEANA MANENO MAKALI NA HAWAJAWAHI KUGUSWA HATA SIKU MOJA??

KUNA MMOJA WENU ALIYEKUWA NA OPTION B, AMBAYO NI YA WATU WENYE WAKE ZAO, WATOTO, WAJUKUU, DADA, KAKA AU WAJOMBA NA MASHANGAZI HUKO HOSPITALINI WASIOTIBIKA KWA SABABU ZA DK. ULIMBOKA???

MGOMO WA MADAKITARI UMEZIDI HAPA NCHINI, WAMEKUWA WAKIZIWEKA ROHO ZETU REHANI KWA MUDA MREFU SANA, ITS ABOUT TIME SEREKAI ITOE MAAMUZI MAGUMU.

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA

DKT NCHIMBI AZURU KABURI LA JOHN KOMBA LITUHI, NYASA