KINANA AITESA CHADEMA NA KUWAITA MADIKTETA

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye kiwanja cha ndege mjini Mogogoro leo, kuhitimisha ziara kikazi ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua kiradi ya maendeleo kwa wilaya zote za mkoa hu

Na Mwandishi Wetu,Morogoro

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Abdulrahman Kinana amekichambua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), na kukifananisha na madikteta, wanaojali maslahi yao si wananchi.

Amesema viongozi wa chama hicho wamekuwa madiktekta wakubwa na wao ndio wanajiona wanajua kila jambo kuliko watu wengine na ikitokea mtu wa upinzani ameipongeza serikali kwao huonekana msaliti na kibaraka wa CCM.

Akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika leo mjini hapa,Kinana, amesema kuwa Chadema ni hatari kwa Taifa na watu kwani viongozi wake wamekuwa ni watu wa kuhubiri machafuko badala ya mshikamanokwa Watanzania.

Alisema kutokana na unafsi wao huo hivi sasa chama hicho kimeanza kuigawa nchi kwa kutumia ukanda na sera yao ya ukanda kinyume cha katiba ya nchi na watu wake.

"Ndugu zangu Watanzania ninapenda leo niwaelezeni namna Chadema ilivyojawa na ubinafsi ambapohivi sasa wamekuwa wakiwakukusanya Watanzania na kuwagawa kwa sera yao ya majimbo. hili si mara ya kwanza maana katika kipindi cha siku za hivi karubuni walitangaza wazi kuigawa nchi kwa kutaka kujitenga kanda ya Kaskazini ambayo itakuwa chini ya utawala wao.

"CCM kama chama kilichoingia mkataba na watanzania katu haiwezi kukaa kimya na kuona hali hii ikitokea, kila mara tumekuwa tukihubiri amani na mshjkamano lakini wenzetu hili limewashinda na sasa wameingia katika kuwagawa watanzania.

"Katu CCM itaendelea kusema ukweli kwa kila jambo na hawa Chadema muwe nao makini hasa kutokana na aina ya siasa na matendo yao wanayoyafanya sasa," alisema Kinana.


Vurugu za Chadema Kinana alisema kuwa Chadema wamekuwa ni watu wa maajabu na vurugukubwa nchini, na katika hilo alitoa mfano ya mambo ambayo wanayafanya bungeni.

"Chadema kazi yao ni vurugu tu, utadhani wao ndio wamekuwa wapinzani katika nchi .Walikuwepo wapinzani kabla yao lakini kwa sasa wanajiona wao ndio kila kitu.Wanatoa vitisho kila siku kwa Serikali.

"Wanabeza wapinzani wengine , wakiona mpinzani anapongeza kazi iliyofanywa na CCM wanaanza kumshambulia.Hakuna anayejua zadi yaChadema .Wanamtukana Rais, wanaushambulia usalama wa  Taifa, wanashambulia vyombo vya usalama,"alisema Kinana

"Hawa jamaa ni watu wa ajabu sana, kila kitu wanajua wao wengine hawajui.Wakigombana katika chama chao utasikia kuna mkono wa CCM.Sijui ni watu wa aina gani , wanafanya mambo ya ajabu sana,"alisema.

Pamoja na kuichambua Chadema, Kinana aliamua kutoa ushauri kwa Chadema kuwa na uwezo wa kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao kuliko kutumia muda wao mwingi kila jambo ambalo linakwenda kombo kunyoosha vidole kwa CCM.

"CCM tuna changamoto zetu nyingi, lakini tunatatua matatizo yetuwenyewe hatupotayari.Tuna makundi ndani ya chama lakini hayo ndiomambo ya siasa,"alisisitiza.


Mchakato wa Katiba mpya Kinana alisema pamoja na kazi nzuri ambayo imefanywa katika mchakato wa Katiba mpya, kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ametoa hotuba yake ambayo inaonesha wazi hakuna ambacho kimefanyika katika mchakato huo.

Alisema kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe akiwa bunge ametumia muda wake mwingi kuzungumzia mchakato wa katiba mpya na kubwa katika hotuba yake kuwa haufai.

"Simsingizii kiongozi wa Kambi ya upinzani bungeni, ndani ya hotuba yake ameeleza wazi kuwa waliopewa dhamana ya kukusanya maoni ya Katiba mpya hawana ujuzi.Hii si kweli, waliopewa dhamana hiyo ni watu ambaowanaifanya kazi hiyo kwa uadilifu,"alisema.

Alisema Chadema ni watu binafsi ambao wao wametawaliwa na uroho mkubwa na wao kazi ni kuangalia maslahi zaidi na ni si maslahi ya nchi.Ziara yake Morogoro

Kinana alisema kuwa ziara yake amejifunza mamb mengi lakini kubwa na amsingi ambalo lipo kwa chama hicho kitahakikisha kinatafuta ufumbuzi wa matatizo ya wananchi na hasa migogoro ya ardhi, mipaka na huduma za jamii ambazo nazo ni changamoto kubwa kwa maeneo mbalimbali.

"Ziara yangu na viongozi wengine wa chama chetu ambayo tuimefanya katika wilaya zote za Morogoro tumeona changamoto nyingi.Tumetafuta ufumbuzi wa matatizo lakini mengine yanapatiwa ufumbuzi baada ya kukaa na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama na kisha kutoa maagizo kwa Serikali kutekeleza,"alisema.

Agizo kwa wabunge CCM Katibu Mkuu huyo wa CCM, alitumia nafasi hiyo kwa kuwataka wabunge wa CCM kutembea kifua mbele kwani chama chao kinafanya kazi kubwa lakini aliwataka wawe makini na Chadema na kuwataka kutowasikiliza kwani sasa imetosha.

Alisema Chadema wamekuwa wakisikiliza muda mrefu ndani ya Bunge na kuna wakati wabunge wa CCM walichukia baada ya Rais Jakaya Kikwete kukubali kukutana nao kujadili mchakato wa Katiba Mpya.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI