Wabunge waliosimamishwa warejea kwa ari

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Msigwa

Dodoma.
Baada ya kutumikia adhabu ya kutohudhuria vikao vitano vya Bunge, wabunge watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana waliingia bungeni wakionekana kuwa na ari mpya.
Wabunge waliosimamishwa Aprili 17 ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.
Wengine ni Highness Kiwia (Ilemela), Ezekiel Wenje (Nyamagana), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Mbeya Mjini) na Godbless Lema (Arusha Mjini).
Jana asubuhi Mchungaji Msigwa alikuwa miongoni mwa wabunge waliowahi kuingia mapema ndani ya Ukumbi wa Bunge na kufuatiwa na Lissu muda mfupi baada ya kikao kuanza.
Ndani ya Ukumbi wa Bunge, Msigwa alipata nafasi ya kuuliza swali namba 115 lililokuwa liulizwe na Joyce Mukya kuhusu Kampuni ya Kamwene Woodworks . Kwa upande wake, Lissu aliomba mwongozo wa Spika kuhusu kukwama kwa Bajeti ya Wizara ya Maji.
Wabunge wengine haikujulikana sababu za kutofika jana licha ya kuwa adhabu yao ilikwisha tangu April 25 huku taarifa zikieleza kuwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema alikuwa apelekwe mahakamani kujibu staka la uchochezi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI