MMILIKI WA WHATSAPP ALISHAWAHI KUNYIMWA AJIRA KATIKA KAMPUNI YA TWITTER NA FACEBOOK


Waanzilishi wa Whatsapp: Brian Acton na Jan Koum.
Katikati ya mwaka 2009, Brian Acton alikuwa software engineer ambaye hakuna kampuni iliyotaka kumwajiri. Pamoja na uzoefu wa miaka zaidi ya 10 kama mwajiriwa wa Yahoo na Apple Computer, alitosa kuajiriwa kwenye makampuni ya Facebook na Twitter.
Kwanza walikuwa Twitter waliomkataa mwezi May. Tarehe 23, May mwaka 2009, Brian Acton ‏alitweet: Got denied by Twitter HQ. That’s ok. Would have been a long commute.”
Kisha Facebook waliokataa kumchukua mwezi August. Tarehe 3 August, 2009 akatweet: Facebook turned me down. It was a great opportunity to connect with some fantastic people. Looking forward to life’s next adventure.”
Baada ya Acton kukosa kazi kwenye makampuni hayo, aliamua kuanzisha kitu chake mwenyewe. Aliamua kuungana na aliyekuwa mwajiriwa mwenzake wa Yahoo, Jan Koum, kuanzisha WhatsApp, ambayo leo imekuwa mfalme wa mawasialino ya ujumbe duniani. WhatsApp inatawala vichwa vya habari wiki hii sababu Facebook imekubali kuinunua kampuni hiyo kwa dola bilioni 19.


Akiwa na asilimia 20 ya hisa kwenye kampuni, Acton atakuwa tajiri wa dola bilioni 3. Historia yake imegeuka kuwa funzo la watu kutokata tamaa kwa wale wanaotafuta kazi. Story yake pia itawapa uchungu waajiri. Kuajiri watu sahihi ni jambo la bahati lakini hakuna kampuni kubwa duniani itapenda kuwa maarufu kwa kuacha Brian Acton mwingine aondoke.
Chanzo: Forbes

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

BODABODA ALIPWA PIKIPIKI BAADA KUSAFIRI KWA BODA KWA SAA 10 MBEYA HADI DAR

ASANTE GWIJI YAYA TOURE KWA KUPASUA UKWELI UKWELI KUPENDELEWA KWA MOROCCO

CONFIRMED HAWA NDIO WACHEZAJI WETU 12 WA KIGENI 🦾

RAIS WA SENEGAL AWAPATIA ZAWADI NONO WACHEZAJI WALIOFANIKISHA UBINGWA WA AFCON 2025

NYOMI YA WASENEGALI WAKISHANGILIA UBINGWA WA AFCON 2025

'MAREKANI IKIJARIBU KUANZISHA VITA NA URUSI ITAANGAMIA'

TANZANIA YAPANDA VIWANGO VYA FIFA

CCM YAMJIBU BUTIKU CHADEMA KUFUNGIWA