KINANA AWATAHADHARISHA VIONGOZI KUINGIA MIKATABA YA ULAGHAI NA MATAPELI WA ARDHI CHALINZE

 Mjumbe wa Sekretarieti ya Umoja wa Wananwake wa CCM Mkoa wa Pwani, Latifa Kizota akiwa amevaa kilemba chenye picha ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete leo wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika Jimbo la Chalinze, mkoani Pwani.
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akishiriki kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Kata ya Kiwangwa wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kfuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza,akishiriki katika kupigaji lipu katika jengo la upasuaji Kituo cha Afya Miono,
 Kinana akimsikiliza kwa makini mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Miono, Editha Gyindo aliyekuwa akielezea matatizo mbalimbali wanayokabiliana nayo katika shule hiyo, likiwemo la umeme na usafiri
 Kinana akuhutubia katika mkutano katika Kijiji cha Miono leo, ambapo aliwatahadharisha wananchi na viongozi wa eneo hilo kuepukana na matapeli wa mashamba.
 Kinana akimkabidhi msaada wa fedha mama mwenye ulemavu, Amina Saleh aliyekutwa mlangoni baada ya kumaliza kukagua Soko jipya la Mbwewe, katika Jimbo la Chalinze linaloongozwa na Mbunge wa CCM, Ridhiwani Kikwete.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akishiriki kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa jengo la CCM Kata ya Kiwangwa. Anaye mwangalia ni Katibu Mkuu wa CCM,  Ndugu Kinana.
 Kinana na Nape wakijadiliana jambo  baada ya kukagua Soko la Mbwewe jimboni Chalinze.
 Kinana akikagua ubao wa moja kati ya vyumba viwilivya madarasa na Makatabavilivyojengwa katika shule ya Msingi Msata kwa msaada wa Taasisi ya Room to Read
 Sehemu ya umati wa wananchi ukimsikiliza Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia mjini Chalinze leo.
 Kinana akuhutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chalinze leo, ambapo aliwataka viongozi  wawe makini kuepukana na matapeli wa ardhi wanaojitokeza kwa wingi sasa na kuwatapeli wananchi.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo,Shukuru Mbato akijibu moja ya maswal;i aliyoulizwa na wananchi mbele ya Kinana katika mkutano huo wa hadhara.
 Mfugaji mwenye jamii ya Kimasai, Chagwa Said wa Kijiji cha Vigwaza akiuliza swali kuhusu haki ya wafugaji katika eneo hilo.Pia alielezea jinsi tabia ya rushwa ilivyokithiri.
 Mama Mwangali Kisosi akielezea mbele ya Kinana jinsi alivyodhulumiwa fidia ya nyumba , shamba na makaburi na taasisi ya Mwenge iliyokubaliana naye kwamba kabla ya kuhamishwa angelipwa fidia lakini hadi sasa hajalipwa.
Kinana akisalimiana na baadhi ya viongozi wa matawi ya CCM Jimbo la Chalinze waliopatiwa baiskeli kwa ajili ya kurahisisha utendaji. Baiskeli hizo zimetolewa msaada na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.